📰 Newspapers

Sababu za Ruto kuenda Congo ghafla usiku

Sababu za Ruto kuenda Congo ghafla usiku

RAIS William Ruto na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi, wamepata fursa mpya ya kurekebisha uhusiano wa kidiplomasia uliodorora kati ya nchi zao kwa karibu miaka mitatu.

Viongozi hao walikutana Jumapili katika mkutano wa viongozi wanne uliofanyika Oyo, Jamhuri ya Congo, pamoja na Rais wa nchi hiyo Denis Sassou-N’Guesso na kiongozi wa Togo Faure Gnassingbé.

Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kikanda, usalama na maendeleo ya kiuchumi.

Dkt Ruto aliwasili Oyo Jumamosi usiku, Novemba 21, 2026, akikatiza ziara yake ya siku nane eneo la Magharibi mwa Kenya.

Katika ujumbe wake, Rais alisema viongozi hao walikuwa na nia ya kuimarisha ushirikiano na kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikumba Afrika.

“Majadiliano yetu yanalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kukuza ushirikiano wa kikanda, kuendeleza amani na usalama na kupanua ushirikiano kwa ajili ya ustawi wa pamoja wa mataifa yetu,” akasema Dkt Ruto.

Kwa upande wake, Rais Tshisekedi alisema mkutano huo ni fursa muhimu ya kujenga upya imani kati ya viongozi wa Afrika na kutafuta suluhu ya kudumu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa DRC.

“Tunajitolea kuimarisha mazungumzo na imani kati ya viongozi wa Afrika na kufanya kazi pamoja kutafuta suluhu za kudumu kwa mzozo wa usalama mashariki mwa DRC. Amani na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu zinahitaji kujitolea kwa pamoja na suluhu zinazoongozwa na Waafrika,” akasema.

In brief

RAIS William Ruto na mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Félix Tshisekedi, wamepata fursa mpya ya kurekebisha uhusiano wa kidiplomasia uliodorora kati ya nchi zao kwa karibu miaka mitatu. Mkutano huo ulilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, ushirikiano wa kikanda, usalama na maendeleo ya kiuchumi. Katika ujumbe wake, Rais alisema viongozi hao walikuwa na nia ya kuimarisha ushirikiano na kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikumba Afrika.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.