📰 Newspapers

Biashara ya magendo yasababishia serikali hasara ya Sh1 trilioni kwa mwaka

Biashara ya magendo yasababishia serikali hasara ya Sh1 trilioni kwa mwaka

MKULIMA wa chai kaunti ya Kiambu anapopeleka majani mabichi katika kituo cha kununua chai, huenda mizani ikaonyesha uzito ulio chini kwa asilimia 14 hadi 20 ya alichovuna.

Huu ni mfano mmoja tu wa biashara haramu ambayo serikali inasema inaletea Kenya hasara ya zaidi ya Sh800 bilioni kila mwaka.

Mitandao hiyo hiyo inayopunguza uzani wa chai ya wakulima pia huuza kemikali bandia, pombe isiyo salama na mbolea feki inayowekwa katika mifuko yenye majina ya bidhaa halisi.

Ripoti mpya ya serikali kuhusu biashara haramu nchini, iliyozinduliwa Mombasa Jumatano, inakadiria kuwa shughuli hizo ziligharimu Kenya Sh826 bilioni mwaka 2018, huku hasara hiyo ikivuka Sh1 trilioni katika miaka iliyofuata.

Katika mwaka huo, hasara hiyo ilikuwa sawa na asilimia 9.3 ya pato la taifa. Serikali pia ilipoteza mapato ya Sh153.1 bilioni, huku ajira 44,198 zikikosekana na uwekezaji wa Sh123 bilioni kutopatikana.

Watengenezaji bidhaa ni miongoni mwa walioathirika zaidi. Ripoti inasema kampuni halali hupoteza wastani wa asilimia 25 ya soko lake, sawa na takriban Sh3.9 milioni kwa mwaka kwa kila kampuni.

Pia, ajira katika kampuni hizo hupungua kwa asilimia 25.5.

Watumiaji nao wako hatarini.

Daktari Robi King’a wa Mamlaka ya Kukabiliana na Bidhaa Bandia alisema hadi asilimia 60 ya baadhi ya aina za pombe na asilimia 89 ya baadhi ya kemikali za kilimo sokoni huenda ni bandia au vimefungwa upya kinyume cha sheria.

In brief

MKULIMA wa chai kaunti ya Kiambu anapopeleka majani mabichi katika kituo cha kununua chai, huenda mizani ikaonyesha uzito ulio chini kwa asilimia 14 hadi 20 ya alichovuna. Ripoti mpya ya serikali kuhusu biashara haramu nchini, iliyozinduliwa Mombasa Jumatano, inakadiria kuwa shughuli hizo ziligharimu Kenya Sh826 bilioni mwaka 2018, huku hasara hiyo ikivuka Sh1 trilioni katika miaka iliyofuata. Katika mwaka huo, hasara hiyo ilikuwa sawa na asilimia 9.3 ya pato la taifa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.