📰 Newspapers

Millie akataa kutumiwa kushambulia Uhuru kufaidi Ruto

Millie akataa kutumiwa kushambulia Uhuru kufaidi Ruto

MBUNGE wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo amesema hana sababu ya kumshambulia rais mstaafu Uhuru Kenyatta ili kupongeza miradi inayotekelezwa na serikali ya sasa inayoongozwa na Rais William Ruto.

Millie asema hataki kujiunga na mijadala ya kisiasa inayomtaka kukosoa tawala zilizopita kila anapotambua mafanikio ya utawala wa sasa.

Akizungumza katika mahojiano na kituo kimoja cha redio Jumatano, Novemba 18, 2026, mbunge huyo alitaja daraja lililojengwa Suba Kaskazini wakati wa utawala wa Uhuru kama mfano wa maendeleo yanayostahili kutambuliwa.

“Watu wanataka nimshambulie Uhuru. Lakini Uhuru alijenga daraja Suba Kaskazini. Kwa kweli, kwa nini nimshambulie?” aliuliza.

Alisema anaweza kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Ruto bila kumkosoa mtangulizi wake.

Millie alisema changamoto za maendeleo nchini haziwezi kulaumiwa kwa serikali moja pekee, akibainisha kuwa tawala zilizopita zimekuwa zikikabiliana na matatizo yanayofanana. Aliongeza kuwa nchi nyingi za Afrika pia zinakabiliwa na changamoto za utawala na maendeleo.

Mbunge huyo pia alihoji matumizi ya fedha katika serikali za kaunti, akisema kiasi kikubwa cha fedha kinachotumwa huko hakionekani kuleta maendeleo yanayotoshana nacho.

Alisema mjadala kuhusu ufisadi umejikita zaidi katika serikali ya kitaifa huku matumizi mabaya ya fedha katika ugatuzi yakipuuzwa.

“Fedha nyingi sana zinatumwa katika kaunti zetu, lakini kuna nini cha kuonyesha?” aliuliza.

Alipendekeza mfumo wa usimamizi na ukaguzi wa miradi ya Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NG-CDF) uweze kutoa mafunzo kuhusu kuimarisha uwajibikaji katika kaunti.

In brief

MBUNGE wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo amesema hana sababu ya kumshambulia rais mstaafu Uhuru Kenyatta ili kupongeza miradi inayotekelezwa na serikali ya sasa inayoongozwa na Rais William Ruto. Lakini Uhuru alijenga daraja Suba Kaskazini. Alisema mjadala kuhusu ufisadi umejikita zaidi katika serikali ya kitaifa huku matumizi mabaya ya fedha katika ugatuzi yakipuuzwa. “Fedha nyingi sana zinatumwa katika kaunti zetu, lakini kuna nini cha kuonyesha?” aliuliza.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.