📰 Newspapers

Ajira za kaunti zimegeuzwa kuwa za jamaa na marafiki, EACC sasa yafichua

Ajira za kaunti zimegeuzwa kuwa za jamaa na marafiki, EACC sasa yafichua

TUME ya Maadili na Kukabili Ufisadi (EACC) imewaonya magavana, madiwani na maafisa wakuu wa serikali za kaunti dhidi ya kuingilia shughuli za kuajiri na kuwapandisha vyeo wafanyakazi.

EACC inasema tabia hiyo inawanyima Wakenya waliohitimu nafasi za ajira wanazostahili.

Tume hiyo inadai kuwa kuna ongezeko la visa vya wanasiasa kuingilia uhuru wa kikatiba wa Bodi za Utumishi wa Umma za Kaunti, huku baadhi yao wakidaiwa kushinikiza kuajiriwa, kuteuliwa na kupandishwa vyeo kwa watu wanaowapendelea.

Kwa mujibu wa EACC, baadhi ya madiwani wanadaiwa kutaka nafasi fulani za kazi zinazotangazwa zihifadhiwe kwa jamaa zao, marafiki na wafuasi wao wa kisiasa.

Wanapewa hisani hizo ili wapunguze shinikizo kwa serikali za kaunti na kulegeza majukumu yao ya kutathmini utendakazi wa magatuzi yao.

Afisa Mkuu wa EACC, Abdi Mohamud alisema uchunguzi wa tume hiyo umebaini kuwa baadhi ya wafanyakazi hupandishwa vyeo kutokana na uhusiano binafsi, mapendeleo ya kisiasa au kutoa hongo badala ya uwezo na utendakazi wao.

“Kuna visa ambapo nafasi za kazi hazitangazwi kupitia ushindani wa haki, au taratibu za kuajiri hupangwa kimakusudi ili kuwafaa jamaa, marafiki, wafuasi wa kisiasa na washirika wa watu wenye ushawishi,” akasema Bw Mohamud.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Meneja wa EACC katika eneo la Magharibi Eric Ngumbi wakati wa uzinduzi rasmi wa ukaguzi wa mifumo ya usimamizi wa rasilimali katika serikali ya Kaunti ya Kakamega, tume hiyo ilisema tabia…

In brief

TUME ya Maadili na Kukabili Ufisadi (EACC) imewaonya magavana, madiwani na maafisa wakuu wa serikali za kaunti dhidi ya kuingilia shughuli za kuajiri na kuwapandisha vyeo wafanyakazi. EACC inasema tabia hiyo inawanyima Wakenya waliohitimu nafasi za ajira wanazostahili. Kwa mujibu wa EACC, baadhi ya madiwani wanadaiwa kutaka nafasi fulani za kazi zinazotangazwa zihifadhiwe kwa jamaa zao, marafiki na wafuasi wao wa kisiasa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.