📰 Newspapers

Natembeya: Babu hana imani kwamba Sifuna atashinda, ndio maana anapanga kuwania 2032

Natembeya: Babu hana imani kwamba Sifuna atashinda, ndio maana anapanga kuwania 2032

GAVANA wa Trans Nzoia George Natembeya sasa anadai kuwa Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino haamini kuwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anaweza kushinda urais 2027 na hana nia ya kuunga azma yake.

Bw Natembeya, ambaye ni mshirika wa karibu wa kisiasa wa Sifuna, anadai kuwa Bw Owino anajipanga kuwania urais 2032 badala ya kumuunga mkono seneta huyo katika azma yake ya kumng'oa Rais William Ruto mamlakani.

Alidokeza kuwa Bw Owino ameahirisha azma yake ya urais hadi 2032 kwa sababu hataki kukabiliana na rais aliye mamlakani katika uchaguzi wa 2027.

Bw Owino, ambaye anaongoza chama cha The Mwananchi Party (TMP), alitangaza Aprili kuwa atawania ugavana wa Nairobi kisha 2027 kwa muhula mmoja kabla ya kuwania urais.

“Nitawania ugavana 2027 kwa muhula mmoja, kisha nitakuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais mnamo 2032,” alisema mnamo Aprili 26.

Akizungumza Jumapili, Bw Natembeya alitilia shaka kujitolea kwa Bw Owino kuunga azma ya Bw Sifuna.

“Babu Owino yuko katika upinzani lakini hayuko Linda Mwananchi,” akasema Bw Natembeya.

Alipoulizwa iwapo Bw Owino anaamini Bw Sifuna anaweza kushinda urais 2027, gavana huyo alisema hesabu za kisiasa za mbunge huyo ndizo zimemfanya kulenga uchaguzi wa 2032.

“Kwa hesabu zake, sisi ni watu wenye akili. Hataki kukabiliana na Rais aliye mamlakani, ndiyo maana anasukuma azma yake hadi 2032,” akasema.

In brief

GAVANA wa Trans Nzoia George Natembeya sasa anadai kuwa Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino haamini kuwa Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna anaweza kushinda urais 2027 na hana nia ya kuunga azma yake. Alidokeza kuwa Bw Owino ameahirisha azma yake ya urais hadi 2032 kwa sababu hataki kukabiliana na rais aliye mamlakani katika uchaguzi wa 2027.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.