📰 Newspapers

Serikali yabanwa kuhusu uwazi wa madini ya Mrima

Serikali yabanwa kuhusu uwazi wa madini ya Mrima

WAKAZI na viongozi wa jamii katika Kaunti ya Kwale wamepinga kutengwa katika mipango ya uchimbaji wa madini adimu na Niobium katika Mrima Hill, yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh8 trilioni.

Jamii hiyo imelalamikia kupata taarifa kuhusu uteuzi wa muungano wa kampuni za Amerika kuendeleza mradi huo kupitia vyombo vya habari, bila kushirikishwa katika maamuzi muhimu.

Ingawa hawapingi uchimbaji, wakazi wanataka serikali iwashirikishe, ifanye tathmini ya kina ya athari za mradi kwa mazingira na jamii, na kuweka wazi namna mapato yatakavyogawanywa kati ya serikali ya kitaifa, kaunti na jamii husika.

Alhamisi iliyopita, Waziri wa Madini, Hassan Joho, alitangaza muungano wa kampuni zilizoshinda zabuni ya kuendeleza uchimbaji huo.

Kwa vizazi vingi, familia zinazoishi maeneo ya Mrima zimekuwa zikitegemea kilimo na ufugaji kujipatia riziki.

Hata hivyo, sasa zinahofia kupoteza mashamba na maeneo ya malisho, kulazimishwa kuhama, mmomonyoko wa udongo na uchafuzi wa vyanzo vya maji.

Aidha, kuna wasiwasi kuwa shughuli hizo zinaweza kuharibu maeneo ya kitamaduni na madhabahu yanayochukuliwa kuwa matakatifu na jamii.

Mzee wa Kaya, Masudi Mwarezo, alisema jamii haijashirikishwa ipasavyo licha ya Katiba kutaka wananchi washirikishwe katika maamuzi yanayowaathiri.

Alionya kuwa huenda wakazi wakanyimwa manufaa ya kiuchumi, kama walivyodai kutokea wakati wa shughuli za kampuni ya Base Titanium.

Alitaja vijiji vitano vya Bumbuni, Herani, Mwabovo, Dzuni na Mwachanongo, vinavyojulikana kama Lango la Baraka, kuwa miongoni mwa maeneo yatakayoathiriwa.

In brief

WAKAZI na viongozi wa jamii katika Kaunti ya Kwale wamepinga kutengwa katika mipango ya uchimbaji wa madini adimu na Niobium katika Mrima Hill, yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh8 trilioni. Jamii hiyo imelalamikia kupata taarifa kuhusu uteuzi wa muungano wa kampuni za Amerika kuendeleza mradi huo kupitia vyombo vya habari, bila kushirikishwa katika maamuzi muhimu. Aidha, kuna wasiwasi kuwa shughuli hizo zinaweza kuharibu maeneo ya kitamaduni na madhabahu yanayochukuliwa kuwa matakatifu na jamii.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.