📰 Newspapers

Ubishi wachacha ODM kuhusu kumwekea Ruto masharti ya ushirikiano kwa uchaguzi 2027

Ubishi wachacha ODM kuhusu kumwekea Ruto masharti ya ushirikiano kwa uchaguzi 2027

CHAMA cha ODM kinakabiliwa na mgawanyiko kuhusu masharti kinayopaswa kuweka kabla ya kuingia katika makubaliano rasmi ya kisiasa na Rais William Ruto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.

Baadhi ya viongozi wanataka chama hicho kiwe na makubaliano ya maandishi yatakayokihakikishia mgao mkubwa serikalini na kulinda ngome zake za kisiasa, huku wengine wakionya kuwa kumwekea Rais masharti makali kunaweza kuhatarisha ushirikiano wao.

Tofauti hizo zilijitokeza wazi Ijumaa wakati wa mazishi ya Joshua Orero, kakake Mbunge wa Kibra Peter Orero, ambapo viongozi walitoa misimamo tofauti kuhusu uhusiano wa ODM na Rais Ruto.

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, alikosoa viongozi wanaosisitiza masharti makali, akisema chama kinapaswa kuzingatia maendeleo yanayotekelezwa na serikali badala ya kutanguliza nyadhifa.

“Ni kweli tunapaswa kuimarisha chama, lakini tuwe waangalifu tunapofanya hivyo. Tusivifanye vyama vingine kuwa maadui wetu kwa sababu mwishowe sote tunaweza kupoteza katika hali hiyo,” akasema Dkt Omollo.

Katibu huyo alisema wakazi wanapaswa kutathmini miradi ya maendeleo ya serikali badala ya kujikita katika mazungumzo ya kugawana mamlaka.

Hata hivyo, Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga alisisitiza kuwa ODM haiwezi kuingia katika muungano bila masharti ya wazi yanayojulikana.

“Kama chama na jamii, lazima tujadiliane kuhusu mamlaka na kuamua viti tutakavyopata. Tukiingia katika ushirikiano bila mazungumzo, tutakuwa tunadanganyana,” akasema.

Bi Wanga alisema uhusiano wa ODM na Rais Ruto umekuwa mzuri, akifichua kuwa kiongozi huyo wa taifa ametembelea…

In brief

CHAMA cha ODM kinakabiliwa na mgawanyiko kuhusu masharti kinayopaswa kuweka kabla ya kuingia katika makubaliano rasmi ya kisiasa na Rais William Ruto kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Hata hivyo, Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga alisisitiza kuwa ODM haiwezi kuingia katika muungano bila masharti ya wazi yanayojulikana. Tukiingia katika ushirikiano bila mazungumzo, tutakuwa tunadanganyana,” akasema.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.