📰 Newspapers

Hesabu ngumu kwa Babu ugavana wa jiji

Hesabu ngumu kwa Babu ugavana wa jiji

MBUNGE wa Embakasi Mashariki Babu Owino sasa amejipata katika hali ngumu ya kutimiza azma yake ya kuwa gavana kutokana na cheche kali kati yake na Kiongozi wa Linda Mwananchi Edwin Sifuna.

Bw Owino ana kibarua kigumu katika siasa za jijini huku mikakati ikiendelea kusukwa pia na mrengo wa DCP ambao Kinara wake Rigathi Gachagua alitangaza kuwa gavana mpya wa jiji atatoka chama hicho.

Wiki hii, Bw Sifuna alimkabili vikali Bw Owino kuhusu uongozi wa chama cha Linda Mwananchi (LMM) akikanusha kuwa hakumsaliti mbunge huyo katika mpangilio wa uongozi ambao wawili hao walikuwa nao.

“Katika vyama vyote vilivyoko nchini, nitajie chama kimoja ambacho mgombeaji urais si kiongozi wake,” akauliza Bw Sifuna.

“Mlipokuwa mkibishana kuhusu nani awe kiongozi wa chama, niliwauliza, mnawezaje kuniamini niwe rais wa nchi lakini msiniamini kuwa kiongozi wa chama? Sasa msaliti ni nani?”

Alikuwa akikanusha matamshi ya Bw Owino kuwa walikubaliana kuwa Bw Sifuna angekuwa mgombeaji wa urais huku naye mbunge huyo akiongoza chama ambacho wangekiunda.

Kwa sasa Bw Owino yuko katika chama cha Mwananchi (TMP) ambacho alikichukua kutoka kwa aliyekuwa Gavana wa Makueni Profesa Kivutha Kibwana.

Kando na kutangaza kuwa atawania ugavana kupitia chama hicho, Bw Owino pia anapanga kuwasilisha wagombeaji wa udiwani kupitia chama hicho si Nairobi pekee bali kote nchini.

Ingawa hivyo, tangu 2013 walioshinda ugavana wamekuwa wakitoka kwenye vyama vikubwa.

In brief

MBUNGE wa Embakasi Mashariki Babu Owino sasa amejipata katika hali ngumu ya kutimiza azma yake ya kuwa gavana kutokana na cheche kali kati yake na Kiongozi wa Linda Mwananchi Edwin Sifuna. “Katika vyama vyote vilivyoko nchini, nitajie chama kimoja ambacho mgombeaji urais si kiongozi wake,” akauliza Bw Sifuna. Alikuwa akikanusha matamshi ya Bw Owino kuwa walikubaliana kuwa Bw Sifuna angekuwa mgombeaji wa urais huku naye mbunge huyo akiongoza chama ambacho wangekiunda.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.