📰 Newspapers

KINAYA: Mwanasiasa anayekuahidi utajiri ni tapeli!

KINAYA: Mwanasiasa anayekuahidi utajiri ni tapeli!

NITAKUTAJIRISHA’ au ‘nitatia pesa mfukoni mwako’ ni lugha ya waganga na matapeli!

Naam, ukiyasikia maneno hayo tu gusa mfuko wako ili uhakikishe uko salama, lau sivyo uishie ‘ningalijua’.

Labda umeibiwa hata nauli. Huenda ukachanganya nyayo hadi nyumbani.

Muepuke kama jini au shetani mwanasiasa yeyote anayekwambia umchague au umpe fursa ya kukuongoza kwa muhula wa pili ili akutajirishe.

Anataka kukuangamiza kiuchumi. Usihadaike kitoto!

Walio na uzoefu wa kuzuru kilingeni husema mganga atakuahidi nguvu za kiume na labda ameachwa na mkewe kwa kupungukiwa kwenye maeneo hayo. Mbona asijitibu kwanza?

Atakuahidi kukutajirisha, lakini dalili ziko wazi kwamba hata yeye anahangaika.

Mbona amewahudumia watu miaka yote hii na hajastaafu mapema kwa sababu pesa zimetosha, angaa akapunge upepo ufukweni na ‘kurudishia mwili shukrani’?

Kwa nini asifanye ‘dili’ moja kali pale kilingeni, atajirike mara moja, aache kukesha akikupigia ramli na mambo mengine machafu na ya kishetani kama hayo?

Mbona amekuwa kama bango linalokuelekeza kwa kwenda, lakini kamwe haliendi huko? Kwani yeye hataki kutajirika?

Mambo haya si mageni mjini! Ahadi za kukutajirisha zimekaririwa na wanasiasa tangu zamani. Je, umetajirika? Umeegesha gari lako la kifahari wapi?

Waulize ‘mama mboga’ na vijana wa bodaboda walioahidiwa paradiso na Kasongo wakati wa kampeni za uch-aguzi uliopita iwapo wamefika huko tayari.

Waliahidiwa utajiri kutoka chini hadi juu, kumbe mpango wa hakika ulikuwa kuinuliwa juu, kuinamishwa, kutikiswa ili kila ndururu iliyo mfukoni ianguke…

In brief

NITAKUTAJIRISHA’ au ‘nitatia pesa mfukoni mwako’ ni lugha ya waganga na matapeli! Atakuahidi kukutajirisha, lakini dalili ziko wazi kwamba hata yeye anahangaika. Kwa nini asifanye ‘dili’ moja kali pale kilingeni, atajirike mara moja, aache kukesha akikupigia ramli na mambo mengine machafu na ya kishetani kama hayo? Mbona amekuwa kama bango linalokuelekeza kwa kwenda, lakini kamwe haliendi huko?

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.