📰 Newspapers

Afisa wa polisi aliyemhudumia Uhuru apandishwa cheo na Ruto

Afisa wa polisi aliyemhudumia Uhuru apandishwa cheo na Ruto

AFISA mkuu wa usalama aliyekuwa akimhudumia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, Pepita Ranka, amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Mipango katika makao makuu ya polisi, Vigilance House, Nairobi.

Bw Ranka, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais wakati wa utawala wa Bw Kenyatta, anachukua nafasi ya Peter Ndung’u aliyestaafu Novemba 13, 2026.

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi nchini (DCI) Mohammed Amin amefanya mabadiliko katika kikosi maalum cha Operations Support Unit (OSU), akimteua David Chebii kuwa naibu mkuu wake.

Bw Amin pia ameamuru shughuli zote za kikosi hicho kuhamishiwa makao makuu ya DCI, Barabara ya Kiambu.

OSU iliundwa baada ya Rais William Ruto kuvunja Special Service Unit (SSU) mnamo 2022 kufuatia madai ya kuhusika kwa maafisa wake katika utekaji nyara na mauaji ya raia watatu, wakiwemo wawili wenye asili ya Kihindi.

Kikosi hicho kipya pia kimekabiliwa na madai ya utekaji nyara na ukiukaji wa haki za binadamu, hasa wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Serikali imekanusha kuwepo kwa kikosi cha polisi kinachotekeleza mauaji ya kiholela, ikisisitiza kuwa maafisa wote wanapaswa kutii sheria.

In brief

AFISA mkuu wa usalama aliyekuwa akimhudumia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, Pepita Ranka, amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Masuala ya Mipango katika makao makuu ya polisi, Vigilance House, Nairobi. Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi nchini (DCI) Mohammed Amin amefanya mabadiliko katika kikosi maalum cha Operations Support Unit (OSU), akimteua David Chebii kuwa naibu mkuu wake. Serikali imekanusha kuwepo kwa kikosi cha polisi kinachotekeleza mauaji ya kiholela, ikisisitiza kuwa maafisa wote wanapaswa kutii sheria.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.