📰 Newspapers

Wakulima Magharibi wamwagiwa Sh1.2 bilioni na Rais Ruto

Wakulima Magharibi wamwagiwa Sh1.2 bilioni na Rais Ruto

RAIS William Ruto alianza kusambaza bonasi ya Sh1.2 bilioni kwa wakulima wa miwa katika eneo la Magharibi mwa Kenya jana, huku akiahidi kuongeza maradufu malipo hayo mwakani ili kuimarisha kilimo cha miwa nchini.

Jana, Rais alikabidhi hundi za bonasi za Sh195 milioni kwa wakulima wa miwa wa kiwanda cha sukari cha Nzoia, huku akitangaza kuwa wenzao wanaosambaza mazao yao katika kiwanda cha Mumias watapokea malipo yao wiki ijayo.

Wakulima wa Chemelil, Muhoroni, Miwani na Sony pia wanatarajiwa kunufaika na bonasi hizo.

Akizungumza katika uwanja wa kiwanda cha Nzoia Sugar, eneobunge la Kanduyi, Kaunti ya Bungoma, katika siku ya nne ya ziara yake Magharibi, Rais alisema malipo hayo ni ishara ya kutimizwa kwa ahadi yake ya kufufua sekta ya sukari na kilimo cha miwa.

Alisema kukodishwa kwa kiwanda hicho kwa kampuni ya Rai Group kumebadilisha shughuli zake na kukirejesha katika hali ya kupata faida baada ya kukaribia kusambaratika miaka mitatu iliyopita.

“Miaka minne iliyopita tuliposimama katika uwanja huu na kuahidi kufufua kiwanda hiki, kilikuwa miongoni mwa viwanda visivyo na ufanisi zaidi. Leo wakulima wanalipwa ndani ya wiki moja baada ya kuwasilisha miwa, huku wafanyakazi wakipokea mishahara yao kwa wakati kila mwisho wa mwezi. Hii ni siku ya kihistoria kwa Nzoia Sugar,” akasema.

Rais alisisitiza kuwa kiwanda hicho na shamba lake kuu la miwa bado ni mali ya wananchi wa Bungoma, akipuuza…

In brief

RAIS William Ruto alianza kusambaza bonasi ya Sh1.2 bilioni kwa wakulima wa miwa katika eneo la Magharibi mwa Kenya jana, huku akiahidi kuongeza maradufu malipo hayo mwakani ili kuimarisha kilimo cha miwa nchini. Jana, Rais alikabidhi hundi za bonasi za Sh195 milioni kwa wakulima wa miwa wa kiwanda cha sukari cha Nzoia, huku akitangaza kuwa wenzao wanaosambaza mazao yao katika kiwanda cha Mumias watapokea malipo yao wiki ijayo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.