📰 Newspapers

Wakenya wanaoishi Amerika wamwahidi Sifuna mamilioni kufadhili kampeni zake

Wakenya wanaoishi Amerika wamwahidi Sifuna mamilioni kufadhili kampeni zake

KIONGOZI wa Linda Mwananchi Movement (LMM) Edwin Sifuna ameanzisha harakati za kutafuta ufadhili wa kampeni zake za urais za 2027 nchini Amerika, huku akiwahimiza Wakenya wanaoishi ughaibuni kuchangia azma yake ya kuingia Ikulu.

Barua zilizowasilishwa katika Idara ya Haki, Amerika zinaonyesha kuwa Mkenya anayeishi New Jersey, Dkt Gilbert Shanga, aliomba Oktoba 28 kuratibu ziara ya Seneta huyo wa Nairobi.

Dkt Shanga alipewa jukumu la kufanikisha mikutano ya Bw Sifuna na Wakenya wanaoishi Amerika Kaskazini pamoja na kuratibu shughuli za kuchangisha fedha.

Bw Sifuna na ujumbe wa wanasiasa wanaounga mkono azma yake waliwasili Amerika mnamo Novemba 20 kwa ziara itakayokamilika Disemba 7 kwa chakula cha jioni Silicon Valley.

Katika mkutano na Bw Sifuna, Mkenya anayeishi North Carolina, George Njue, aliahidi kuhamasisha wananchi wanaoishi ughaibuni kuchangisha Sh100 milioni kwa kampeni zake.

Bw Njue, ambaye alisema aliendesha gari kwa saa tisa kuhudhuria mkutano huo, alihimiza Wakenya Amerika kujiunga na juhudi za kifedha za LMM.

“Hamna Wakenya wengi ughaibuni kama ya Amerika. Tuna pesa zote zinazohitajika na Linda Mwananchi kumfanya Sifuna kuwa rais,” alisema.

Alisema Wakenya ughaibuni wanatarajia watanufaika kiuchumi kupitia miradi ya maendeleo iwapo Bw Sifuna atashinda urais.

Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga, ambaye ni mshirika wa karibu wa Bw Sifuna, alisema Bw Njue ameahidi kutoa fedha hizo kabla ujumbe huo haujaondoka Amerika.

In brief

KIONGOZI wa Linda Mwananchi Movement (LMM) Edwin Sifuna ameanzisha harakati za kutafuta ufadhili wa kampeni zake za urais za 2027 nchini Amerika, huku akiwahimiza Wakenya wanaoishi ughaibuni kuchangia azma yake ya kuingia Ikulu. “Hamna Wakenya wengi ughaibuni kama ya Amerika. Alisema Wakenya ughaibuni wanatarajia watanufaika kiuchumi kupitia miradi ya maendeleo iwapo Bw Sifuna atashinda urais.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.