📰 Newspapers

Familia zalilia fidia na hatima yao uchimbaji mafuta ukianza Turkana

Familia zalilia fidia na hatima yao uchimbaji mafuta ukianza Turkana

FAMILIA za wafugaji katika eneo la Lokichar Kusini, Kaunti ya Turkana, zimezua maswali kuhusu hatima yao huku serikali ikijiandaa kuanza uchimbaji, usafirishaji na mauzo ya mafuta Desemba 1, 2026.

Familia hizo ambazo zimeishi katika maeneo hayo kwa miaka kadhaa, sasa zinatarajiwa kuondoka kupisha shughuli za uchimbaji mafuta, huku kukiwa na maswali kuhusu fidia, maeneo watakayohamia na mustakabali wa ufugaji wao.

Karibu watu 3,300 wameathiriwa na mradi huo, huku serikali ikitarajia kukamilisha zoezi la fidia katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Wizara ya Fedha ilitangaza hapo awali kuwa imetenga Sh200 milioni kwa awamu ya kwanza ya kulipa fidia kwa wananchi walioathiriwa.

Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi, alisema uchimbaji wa mafuta katika eneo la Amosing-1 ulianza Ijumaa kupitia kampuni ya Gulf Energy, iliyochukua usimamizi wa mradi kutoka Tullow Oil.

Alisema shughuli za uchimbaji zitaendelea bila kusimama na Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua usafirishaji wa mafuta ghafi hadi Bandari ya Mombasa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi wiki ya kwanza ya Disemba.

Meneja wa Kampuni ya Kawi ya Gulf, Franklin Juma, alisema maeneo ya Lopii na Lokwamosing tayari yameanza kupokea malipo ya fidia.

Alisema zaidi ya watu 1,300 kati ya 3,300 walioathiriwa bado hawajapatikana.

Fidia hiyo inasimamiwa na Tume ya Kitaifa ya Ardhi (NLC), Wizara ya Ardhi na Idara ya Petroli, kupitia kamati za usimamizi wa ardhi ya jamii.

In brief

FAMILIA za wafugaji katika eneo la Lokichar Kusini, Kaunti ya Turkana, zimezua maswali kuhusu hatima yao huku serikali ikijiandaa kuanza uchimbaji, usafirishaji na mauzo ya mafuta Desemba 1, 2026. Familia hizo ambazo zimeishi katika maeneo hayo kwa miaka kadhaa, sasa zinatarajiwa kuondoka kupisha shughuli za uchimbaji mafuta, huku kukiwa na maswali kuhusu fidia, maeneo watakayohamia na mustakabali wa ufugaji wao.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.