📰 Newspapers

Makosa katika utungaji wa sentensi katika ngeli ya mahali ya PA-KU-MU

Makosa katika utungaji wa sentensi katika ngeli ya mahali ya PA-KU-MU

LUGHA ya Kiswahili ina ngeli mbalimbali. Ngeli ni kundi la nomino zenye upatanisho wa kisarufi wa namna moja.

Mifano ya ngeli za Kiswahili ni A-WA, KI-VI, YA-YA, LI-YA, U-U, U-ZI, PA-KU-MU. Ili sentensi iwe sahihi, sharti mtu azingatie upatanisho faafu wa kisarufi.

Kuna mazoea ya kuchanganya viashiria na viambishi vya ngeli ya PA-KU-MU katika sentensi moja.

Mara kwa mara utapata sentensi kama vile: *Shambani pale kumepandwa miche. *Shimoni mle pameingia panya mkubwa. *Sokoni kule pana bidhaa nyingi.

Ujumbe katika sentensi hizi unaeleweka. Hata hivyo, sentensi hizi si sahihi. Hazijazingatia upatanisho unaofaa wa kisarufi.

Ngeli ya PA-KU-MU hujumuisha nomino za mahali. Silabi PA- huashiria mahali panapojulikana.

Silabi KU- huashiria mahali pasipojulikana na silabi MU – huashiria mahali ndani.

Ni kosa kutumia viashiria na viambishi vyote vya PA-KU-MU katika sentensi moja kwani sentensi hiyo itachanganya mahali panapozungumziwa.

Ikiwa sentensi inarejelea mahali panapojulikana, sharti vivumishi na viambishi vya vitenzi vianze kwa pa-, Ikiwa ni mahali pasipojulikana kiambishi cha nomino kwenye kitenzi kianze kwa ku-, Iwapo ni mahali ndani sharti kiambishi kitenzi kiwe m-.

Ili kukosoa mifano hiyo ya sentensi tunafaa kusema: Shambani pale pamepandwa miche. Shimoni mle mmeingia panya mkubwa. Sokoni kule kuna bidhaa nyingi.

Mwanafunzi mwenye changamoto ya kutunga sentensi akitumia nomino za ngeli ya PA-KU-MU anafaa kwanza atambue nomino katika ngeli ya PA-KU-MU kisha afanye mazoezi ya kuandika sentensi sahihi akitumia…

In brief

LUGHA ya Kiswahili ina ngeli mbalimbali. Ujumbe katika sentensi hizi unaeleweka. Silabi KU- huashiria mahali pasipojulikana na silabi MU – huashiria mahali ndani. Ni kosa kutumia viashiria na viambishi vyote vya PA-KU-MU katika sentensi moja kwani sentensi hiyo itachanganya mahali panapozungumziwa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.