📰 Newspapers

Familia za watu wawili waliotekwa nyara zahangaika

Familia za watu wawili waliotekwa nyara zahangaika

FAMILIA za wanaume wawili waliotekwa nyara katika visa tofauti Mombasa na Lamu zimeendelea kukosa majibu kuhusu waliko wapendwa wao baada ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kusema haijawazuilia.

Hata hivyo, Mahakama Kuu ya Mombasa imeagiza maafisa wa usalama kukamilisha uchunguzi na kuwasilisha ripoti kamili ndani ya siku tatu kuhusu kutoweka kwa Ismail Yusuf Mohamed na Ali Kassim.

Mohamed alitekwa eneo la Bondeni karibu na Camels Joint usiku wa Oktoba 30 mwaka huu akitafuta chakula.

Kwa mujibu wa DCI, kisa hicho kiliripotiwa katika kituo cha polisi cha Central mnamo Oktoba 31 na Fatuma Saidi.

Polisi walisema uchunguzi ulianza katika kituo hicho kabla ya kuhamishiwa kwa DCI Urban Police Station, huku taarifa za kutafuta Mohamed zikitumwa katika vituo vya polisi kote nchini.

Hata hivyo, DCI ilisema baadhi ya mashahidi wanaohusishwa na tukio hilo hawajapatikana na uchunguzi wa kamera za CCTV bado unaendelea.

Shirika la Vocal Africa, ambalo limewasilisha kesi kwa niaba ya Mohamed, linadai kuwa kamera zilirekodi watu waliokuwa wakimfuatilia kwa gari aina ya pickup kabla ya kumteka na kumuingiza katika Toyota Land Cruiser nyeupe.

Shirika hilo linataka Inspekta Jenerali wa Polisi amfikishe Mohamed mahakamani akiwa hai au amekufa na kueleza aliko.

Mohamed aliwahi kushtakiwa kwa kosa la kuajiri watu kwa ajili ya kundi la kigaidi, lakini aliachiliwa huru na mahakama ya Malindi Agosti 11, 2023 baada ya upande wa mashtaka…

In brief

FAMILIA za wanaume wawili waliotekwa nyara katika visa tofauti Mombasa na Lamu zimeendelea kukosa majibu kuhusu waliko wapendwa wao baada ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kusema haijawazuilia. Polisi walisema uchunguzi ulianza katika kituo hicho kabla ya kuhamishiwa kwa DCI Urban Police Station, huku taarifa za kutafuta Mohamed zikitumwa katika vituo vya polisi kote nchini.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.