📰 Newspapers

Korti yakataa ombi jipya la kumzuia Sonko kuongoza chama cha NEDP

Korti yakataa ombi jipya la kumzuia Sonko kuongoza chama cha NEDP

ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Mike Sonko, ataendelea kuhudumu kama kiongozi wa chama cha National Economic Development Party (NEDP) baada ya Mahakama Kuu kukataa kwa mara ya pili ombi la kumzuia kushikilia wadhifa huo.

Jaji Roselyne Aburili alikataa ombi jipya lililowasilishwa na wakili Nick Sanare, aliyetaka Sonko azuiwe kutumia mamlaka ya kiongozi wa chama hicho hadi kesi inayopinga ufaafu wake iamuliwe.

Wakili huyo pia anataka Msajili wa Vyama vya Kisiasa azuiwe kumtambua au kumchapisha Sonko kwenye Gazeti Rasmi la Serikali kama kiongozi au afisa wa NEDP.

Mzozo huo unatokana na swali kuhusu iwapo kuondolewa kwa Sonko katika wadhifa wa ugavana kupitia mchakato wa kumng'oa madarakani kunamnyima kikatiba nafasi ya kuongoza chama cha kisiasa.

Bw Sanare anasema kuondolewa kwa Sonko kunamzuia kushikilia wadhifa wowote katika uongozi wa chama chini ya Sura ya Sita ya Katiba na Sheria ya Vyama vya Kisiasa.

Anategemea Kifungu cha 75(3) cha Katiba, kinachoweka masharti kuhusu mtu aliyeondolewa madarakani kwa kukiuka maadili ya uongozi kushikilia wadhifa mwingine wa serikali.

Pia anataka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) izuiwe kupokea vyeti vya uteuzi, orodha za wagombeaji au stakabadhi nyingine zitakazotiwa saini na Sonko akiwa kiongozi wa NEDP.

Katika kesi hiyo, anadai Sonko alianzisha chama hicho kilichosajiliwa Desemba 9, 2025, na ameendelea kutekeleza majukumu ya uongozi, yakiwemo kuwasilisha wagombeaji katika chaguzi ndogo.

In brief

ALIYEKUWA Gavana wa Nairobi Mike Sonko, ataendelea kuhudumu kama kiongozi wa chama cha National Economic Development Party (NEDP) baada ya Mahakama Kuu kukataa kwa mara ya pili ombi la kumzuia kushikilia wadhifa huo. Katika kesi hiyo, anadai Sonko alianzisha chama hicho kilichosajiliwa Desemba 9, 2025, na ameendelea kutekeleza majukumu ya uongozi, yakiwemo kuwasilisha wagombeaji katika chaguzi ndogo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.