📰 Newspapers

Serikali yachunguza madai ya udukuzi wa jukwaa la eCitizen

Serikali yachunguza madai ya udukuzi wa jukwaa la eCitizen

SERIKALI imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya shambulizi kubwa la kimtandao dhidi ya mfumo wa eCitizen, huku kukiwa na hofu kuwa taarifa binafsi za Wakenya na data za serikali huenda ziliibwa.

Kundi la wahalifu wa kimtandao linalojiita ByteToBreach linadai kuwa lilidukua mfumo huo na kuiba gigabaiti 600 za stakabadhi za taarifa za wateja, gigabaiti 100 za data na gigabaiti 40 za misimbo ya programu za kompyuta.

Taarifa hizo ziliibuliwa Jumatatu na kampuni ya Amerika inayohusika na usalama wa kimtandao, Vecert.

Kundi hilo pia linadai kuwa liliweza kuingilia mifumo inayowaunganisha Wakenya na huduma mbalimbali za serikali.

Hata hivyo, Wizara ya Usalama wa Ndani ilisema kikosi chake cha kiufundi na usalama kinafanya uchunguzi kubaini ukubwa wa tukio hilo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, wizara hiyo ilihakikishia umma kuwa huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana kama kawaida.

“Tunashirikiana na mashirika husika ya serikali kukabiliana na tukio hili. Huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana na umma unaweza kuendelea kuzitumia kama kawaida," ilisema wizara.

Kampuni ya Webmasters Kenya Ltd, inayosimamia jukwaa la eCitizen, iliambia ‘Taifa Leo’ kuwa suala hilo linashughulikiwa na mashirika husika ya serikali.

eCitizen ni jukwaa kuu linalowawezesha Wakenya na wakazi wengine kupata huduma za serikali kupitia akaunti moja.

Jukwaa hilo linaunganisha zaidi ya huduma 22,000, zikiwemo maombi ya pasipoti, leseni za udereva, vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa na ndoa, vyeti vya tabia njema na usajili wa biashara.

In brief

SERIKALI imeanzisha uchunguzi kuhusu madai ya shambulizi kubwa la kimtandao dhidi ya mfumo wa eCitizen, huku kukiwa na hofu kuwa taarifa binafsi za Wakenya na data za serikali huenda ziliibwa. Kundi hilo pia linadai kuwa liliweza kuingilia mifumo inayowaunganisha Wakenya na huduma mbalimbali za serikali. Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, wizara hiyo ilihakikishia umma kuwa huduma za eCitizen zinaendelea kupatikana kama kawaida.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.