📰 Newspapers

Kaunti 10 zilizopokea kitita kikubwa cha Sh5 trilioni tangu ugatuzi uanze

Kaunti 10 zilizopokea kitita kikubwa cha Sh5 trilioni tangu ugatuzi uanze

SERIKALI ya kitaifa itakuwa imetuma jumla ya Sh5 trilioni kwa serikali za kaunti kufikia Juni mwakani, miaka 14 tangu mfumo wa ugatuzi kuanzishwa nchini.

Takriban theluthi moja ya fedha hizo zimetengewa kaunti 10 ambazo zimenufaika pakubwa na mfumo huo, zikipokea jumla ya Sh1.6 trilioni kufadhili shughuli za serikali zao na miradi ya maendeleo.

Nairobi imepokea kiasi kikubwa zaidi cha fedha hizo, jumla ya Sh240 bilioni, ikiimarisha nafasi yake kama kaunti yenye mgao mkubwa zaidi nchini.

Hata hivyo, kwa kuzingatia maeneo ya kijiografia, Kaskazini mwa Kenya ndiyo eneo lililonufaika zaidi, huku kaunti tatu zikiingia katika orodha ya 10 zilizopokea fedha nyingi zaidi.

Turkana imepokea Sh167.4 bilioni na kushika nafasi ya pili baada ya Nairobi. Mandera imepokea Sh150.5 bilioni, huku Wajir ikipokea Sh129 bilioni na kushika nafasi ya kumi.

Kwa pamoja, kaunti hizo tatu zimepokea Sh447 bilioni, sawa na takriban asilimia tisa ya fedha zote zilizotengewa kaunti.

Fedha hizo ni karibu mara mbili ya mgao wa Nairobi, licha ya kaunti hizo tatu kuwa na jumla ya wakazi milioni 2.99 mwaka 2025, ikilinganishwa na milioni 4.9 wa Nairobi, kulingana na takwimu za Shirika la Kitaifa la Takwimu (KNBS).

Mkoa wa Magharibi pia umefaidika, huku Kakamega ikipokea Sh164 bilioni na Bungoma Sh140 bilioni.

Kaunti nyingine zilizoingia kwenye orodha hiyo ni Nakuru iliyopokea Sh165.7 bilioni, Kilifi (Sh157.3 bilioni), Kiambu (Sh157 bilioni) na Kitui (Sh135.4 bilioni).

In brief

SERIKALI ya kitaifa itakuwa imetuma jumla ya Sh5 trilioni kwa serikali za kaunti kufikia Juni mwakani, miaka 14 tangu mfumo wa ugatuzi kuanzishwa nchini. Nairobi imepokea kiasi kikubwa zaidi cha fedha hizo, jumla ya Sh240 bilioni, ikiimarisha nafasi yake kama kaunti yenye mgao mkubwa zaidi nchini. Kwa pamoja, kaunti hizo tatu zimepokea Sh447 bilioni, sawa na takriban asilimia tisa ya fedha zote zilizotengewa kaunti.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.