📰 Newspapers

Pigo kwa Netanyahu bunge likiidhisha achunguzwe kuhusiana na shambulio la Hamas

Pigo kwa Netanyahu bunge likiidhisha achunguzwe kuhusiana na shambulio la Hamas

JERUSALEM, Israel: BUNGE la Israel limepiga hatua ya kwanza kuidhinisha mswada wa kuanzisha tume huru ya kuchunguza kushindwa kwa vyombo vya usalama kuzuia shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya taifa hilo. Hatua hiyo ni pigo kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye anapinga uchunguzi huru na badala yake anataka serikali ipewe mamlaka ya kuunda tume na kuteua wajumbe…

JERUSALEM, Israel:

BUNGE la Israel limepiga hatua ya kwanza kuidhinisha mswada wa kuanzisha tume huru ya kuchunguza kushindwa kwa vyombo vya usalama kuzuia shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya taifa hilo.

Hatua hiyo ni pigo kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye anapinga uchunguzi huru na badala yake anataka serikali ipewe mamlaka ya kuunda tume na kuteua wajumbe wake.

Mswada huo ulipata uungwaji mkono wa wabunge 65 dhidi ya 50, huku ukiungwa mkono na kambi ya upinzani inayoongozwa na Gadi Eisenkot pamoja na vyama vinavyowakilisha jamii ya Waarabu.

Hata hivyo, mswada huo unahitaji kupitishwa katika hatua nyingine tatu kabla ya kuwa sheria.

Eisenkot, ambaye anajaribu kuunda serikali mpya baada ya muungano wa Netanyahu kupoteza wingi wa wabunge katika uchaguzi wa Oktoba 27, alisema ukweli lazima ujulikane ili kuzuia maafa kama hayo siku zijazo.

"Kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, manusura wa utumwani na wale ambao hawakurejea wakiwa hai, tutafichua ukweli na kuchukua kila hatua kuzuia janga jingine," akasema katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii.

Netanyahu anapinga tume huru akitaka uchunguzi utakaoongozwa na serikali, huku wapinzani wake wakidai hatua hiyo inalenga kuficha ukweli kuhusu uzembe uliosababisha shambulizi hilo.

"Mswada huu utawachunguza wanajeshi wetu jasiri na mashujaa badala ya kumakinikia masuala ya kimsingi,"

In brief

JERUSALEM, Israel: BUNGE la Israel limepiga hatua ya kwanza kuidhinisha mswada wa kuanzisha tume huru ya kuchunguza kushindwa kwa vyombo vya usalama kuzuia shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023, ambalo lilikuwa baya zaidi katika historia ya taifa hilo. Netanyahu anapinga tume huru akitaka uchunguzi utakaoongozwa na serikali, huku wapinzani wake wakidai hatua hiyo inalenga kuficha ukweli kuhusu uzembe uliosababisha shambulizi hilo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.