📰 Newspapers

Vita vyazuka ndani ya Bunge la Kaunti ya Kisumu wakati wa jaribio la kutimua Spika Oraro

Vita vyazuka ndani ya Bunge la Kaunti ya Kisumu wakati wa jaribio la kutimua Spika Oraro

Vurugu zilitokea katika Bunge la Kaunti ya Kisumu Alhamisi baada ya kundi la madiwani kuanzisha mchakato wa kumuondoa ofisini Spika Elisha Oraro, huku wenzake waliopinga wakijaribu kumlinda.

Mzozo huo uligeuka mapigano ya mateke na makonde, huku Oraro akiondolewa kwa nguvu kutoka kwenye kiti chake.

Tukio hilo lilianza baada ya madiwani kuuliza kwa nini hoja ya kumuondoa spika haikuwa kwenye ratiba ya shughuli za bunge iliyowasilishwa.

MCA wa South West Nyakach Gard Olima na mwenzake wa East Kano Wawidhi Moses Ochele walitaka kujua kwa nini Oraro hakuwa akiongoza kikao kwa kutumia ratiba ya ziada iliyokuwa na hoja hiyo.

Oraro alisema baada ya kushauriana na karani wa bunge, hakuwa amepokea ratiba hiyo ya ziada.

Alisema ataheshimu uamuzi wa madiwani iwapo mchakato wa kumuondoa madarakani utafuata sheria na kanuni za bunge.

Hata hivyo, jibu lake lilizua hasira na kundi la madiwani kuvamia kiti chake na kumtoa kwa nguvu. Baadhi ya waliopinga walijaribu kumkinga, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na mapigano yakazuka.

Maafisa wa polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Kisumu Central walifika kujaribu kurejesha utulivu. Oraro aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi huku baadhi ya wananchi waliokuwa nje ya bunge wakimzomea na kumtishia.

Jaribio lake la kurejea bungeni akiwa ameandamana na polisi lilizimwa na madiwani.

Ochele aliteuliwa kuwa Kaimu Spika na kuongoza kikao kilichofanyika bila karani wala ratiba rasmi ya shughuli za bunge.

In brief

Vurugu zilitokea katika Bunge la Kaunti ya Kisumu Alhamisi baada ya kundi la madiwani kuanzisha mchakato wa kumuondoa ofisini Spika Elisha Oraro, huku wenzake waliopinga wakijaribu kumlinda. Tukio hilo lilianza baada ya madiwani kuuliza kwa nini hoja ya kumuondoa spika haikuwa kwenye ratiba ya shughuli za bunge iliyowasilishwa. Oraro alisema baada ya kushauriana na karani wa bunge, hakuwa amepokea ratiba hiyo ya ziada.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.