📰 Newspapers

Wadau wataka kasi iongezwe katika juhudi za kukomesha ndoa za watoto

Wadau wataka kasi iongezwe katika juhudi za kukomesha ndoa za watoto

ULIMWENGU unapoadhimisha leo Siku ya Kukomesha Ndoa za Watoto, kwa mara ya kwanza baada ya kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa, washikadau wanataka kasi ya juhudi hizo iimarishwe ili kufikia malengo.

Wadau tofauti wakiongozwa na shirika la Femnet, walisema kuwa kwa muda mrefu wameangazia juhudi za kibinafsi, lakini sasa kuna haja ya kuja pamoja na kuelekeza mikakati yao kwa wahusika ili kupata matokeo yatakayosaidia kuzima ndoa za watoto.

Walishiriki warsha hiyo Novemba 26, 2026 katika hoteli ya Park In Radisson, Nairobi.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban wasichana 12 milioni huozwa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.

Kusini mwa Asia ndiko kuna asilimia kubwa ya 44 ya watoto wasichana wanaoozwa mapema, huku Kusini mwa Jangwa la Sahara ikifuata na asilimia 18.

Ingawaje, kulingana na Malengo Endelevu (SDGs), hatua ilikuwa kutimiza lengo hilo kufikia 2030, juhudi hizo zimeonekana kwenda pole pole, na sababu ya wito wa kasi hiyo kuongezwa.

Akiongea katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Femnet Dkt Carole Agengo alisisitiza haja ya mashirika na wadau husika kuungana na kuleta fikra na juhudi zao pamoja ili kuweza kufanikisha lengo hilo.

Mkurugenzi wa Wanawake, Jinsia, na Vijana katika Umoja wa Afrika, Bi Prudence Nonkululeko Ngwenya, pia alishikilia msimamo huo wa kuimarisha juhudi hizo, na watu kuelekea mashinani ambapo matukio hayo yanafanyika na kutafuta suluhu za kudumu.

In brief

ULIMWENGU unapoadhimisha leo Siku ya Kukomesha Ndoa za Watoto, kwa mara ya kwanza baada ya kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa, washikadau wanataka kasi ya juhudi hizo iimarishwe ili kufikia malengo. Ingawaje, kulingana na Malengo Endelevu (SDGs), hatua ilikuwa kutimiza lengo hilo kufikia 2030, juhudi hizo zimeonekana kwenda pole pole, na sababu ya wito wa kasi hiyo kuongezwa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.