📰 Newspapers

Linda Mwananchi yapigwa na baridi bila Sifuna aliye ziarani Amerika

Linda Mwananchi yapigwa na baridi bila Sifuna aliye ziarani Amerika

SAFARI ya Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna nchini Amerika imevuruga kwa muda mikakati ya mrengo wa Linda Mwananchi, ambao ulikuwa umeanza kupata umaarufu kupitia mikutano ya hadhara na shughuli za kujijenga mashinani.

Kutokuwepo kwa Seneta Sifuna, ambaye ndiye sura kuu ya vuguvugu hilo, sasa kunatoa mtihani wa kwanza kuhusu uwezo wa viongozi wake kuendeleza hamasa kwa wafuasi bila yeye kuwepo.

Hali hii inajiri huku Rais William Ruto akizidisha kampeni zake katika eneo la Magharibi mwa Kenya, ambako anaanza ziara ya siku nne kesho.

Sifuna alianza ziara yake Amerika Novemba 20, akikutana na Wakenya wanaoishi ughaibuni kwa lengo la kuchangisha fedha za kufadhili shughuli za kisiasa za Linda Mwananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Ziara hiyo inatarajiwa kukamilika Desemba 7.

Alisafiri na ujumbe wa viongozi kadhaa, akiwemo Mbunge wa Kabuchai Majimbo Kalasinga, aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na mkuu wa mawasiliano wa vuguvugu hilo Pauline Njoroge.

Hata hivyo, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, Mbunge wa Bumula Wanami Wamboka, Mbunge wa Funyula Oundo Mudenyo na aliyekuwa rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) Faith Odhiambo waliachwa nchini.

Mkutano mkubwa wa mwisho wa Linda Mwananchi ulifanyika Ukunda, Kaunti ya Kwale, Oktoba 31.

Tangu wakati huo, shughuli nyingi za vuguvugu hilo zimeonekana kupungua, huku viongozi wake wakisubiri kurejea kwa Sifuna.

In brief

SAFARI ya Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna nchini Amerika imevuruga kwa muda mikakati ya mrengo wa Linda Mwananchi, ambao ulikuwa umeanza kupata umaarufu kupitia mikutano ya hadhara na shughuli za kujijenga mashinani. Sifuna alianza ziara yake Amerika Novemba 20, akikutana na Wakenya wanaoishi ughaibuni kwa lengo la kuchangisha fedha za kufadhili shughuli za kisiasa za Linda Mwananchi kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Tangu wakati huo, shughuli nyingi za vuguvugu hilo zimeonekana kupungua, huku viongozi wake wakisubiri kurejea kwa Sifuna.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.