📰 Newspapers

ODM mambo ni matatu tu kuhusu 2027

ODM mambo ni matatu tu kuhusu 2027

CHAMA cha ODM kinakabiliwa na chaguo tatu: kumuunga mkono Rais William Ruto kuwania muhula wa pili, kuungana na viongozi wa upinzani au kushiriki kivyake katika uchaguzi wa 2027.

Uongozi wa ODM umeweka Januari 31, 2027 kuwa tarehe ya mwisho ya kukamilisha mazungumzo na UDA kuhusu uwezekano wa kuunda muungano rasmi.

Uamuzi huo ulitangazwa Jumatano baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Usimamizi ya chama hicho, huku viongozi wakisema wanataka mazungumzo hayo yakamilike mapema ili kutoa nafasi ya kupanga mikakati ya uchaguzi.

Kiongozi wa wachache katika Bunge la Kitaifa, Junet Mohamed, alisema timu inayoshughulikia sera na manifesto za vyama hivyo itaharakisha kazi ili kutoa ripoti ifikapo Januari 31.

Alisema ripoti hiyo itafafanua masuala na sera zitakazotumika kuunda muungano na UDA.

Hatua hiyo inajiri huku baadhi ya viongozi wa ODM wakilalamikia kutoheshimiwa na kutotambuliwa kwa mchango wa chama hicho katika serikali jumuishi.

Rais Ruto na kiongozi wa ODM Oburu Oginga tayari wameunda kamati ya kiufundi inayolenga kuunganisha manifesto za vyama hivyo kabla ya kutia saini makubaliano rasmi.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge wa Nyanza wanataka Rais Ruto akutane nao haraka ili kujadili masharti ya kumuunga mkono, ikiwemo ugavi wa maeneo ya kisiasa na nafasi ambazo ODM itanufaika nazo.

Mbunge mmoja aliambia Taifa Leo kuwa chama hicho kina wasiwasi kuwa kinaendelea kuunga mkono serikali huku baadhi ya maafisa wakifanya kazi ya kukidhoofisha kisiasa.

In brief

CHAMA cha ODM kinakabiliwa na chaguo tatu: kumuunga mkono Rais William Ruto kuwania muhula wa pili, kuungana na viongozi wa upinzani au kushiriki kivyake katika uchaguzi wa 2027. Hatua hiyo inajiri huku baadhi ya viongozi wa ODM wakilalamikia kutoheshimiwa na kutotambuliwa kwa mchango wa chama hicho katika serikali jumuishi. Mbunge mmoja aliambia Taifa Leo kuwa chama hicho kina wasiwasi kuwa kinaendelea kuunga mkono serikali huku baadhi ya maafisa wakifanya kazi ya kukidhoofisha kisiasa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.