📰 Newspapers

Obado ataangushiwa hukumu ipi? Wazazi wa Sharon wawasili Nairobi kusikiza uamuzi

Obado ataangushiwa hukumu ipi? Wazazi wa Sharon wawasili Nairobi kusikiza uamuzi

WAKAZI wa kaunti za Migori na Homa Bay wanatazamia kwa hamu hukumu itakayotolewa leo, dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado na washirika wake wawili waliopatikana na hatia ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno.

Obado, aliyekuwa msaidizi wake Michael Oyamo na aliyekuwa karani wa kaunti hiyo Caspal Obiero, walipatikana na hatia Julai 23, 2026, baada ya kesi iliyodumu kwa miaka minane.

Katika Kaunti ya Migori, ambako watatu hao walikuwa na ushawishi mkubwa, wakazi wana maoni tofauti kuhusu adhabu wanayostahili.

Baadhi wanataka hukumu kali huku wengine wakitaka mahakama iwaonee huruma.

Hali ni hiyo hiyo Homa Bay, nyumbani kwa Sharon, ambako wazazi na jamaa zake wanasubiri haki itendeke kwa binti yao.

Wazazi wa Sharon wamewasili Nairobi kuhudhuria kikao cha hukumu hiyo.

Baba yake, Douglas Otieno, alisema familia itakubali uamuzi wowote wa mahakama.

“Tulianza safari usiku na kufika asubuhi ili tuweze kufika mahakamani kwa wakati. Kesi hii imedumu miaka minane, ambayo imekuwa mateso kwangu,” alisema.

Mama yake Sharon, Melida Auma, aliomba mahakama Septemba 16 impatie Obado adhabu isiyohusisha kifungo gerezani.

Alisema familia imemsamehe na haitaki ahukumiwe kifo au kifungo cha maisha.

Alisema Sharon aliacha watoto watatu na kumtaka Obado kutimiza ahadi zake za kuwasaidia kupata makazi na mahitaji.

Hata hivyo, wazazi hao walitaka Oyamo na Obiero waadhibiwe kwa mujibu wa sheria.

In brief

WAKAZI wa kaunti za Migori na Homa Bay wanatazamia kwa hamu hukumu itakayotolewa leo, dhidi ya aliyekuwa Gavana wa Migori Okoth Obado na washirika wake wawili waliopatikana na hatia ya mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno. Wazazi wa Sharon wamewasili Nairobi kuhudhuria kikao cha hukumu hiyo. Mama yake Sharon, Melida Auma, aliomba mahakama Septemba 16 impatie Obado adhabu isiyohusisha kifungo gerezani.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.