📰 Newspapers

Masaibu ya Mackenzie yazidi, apatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwanyima chakula

Masaibu ya Mackenzie yazidi, apatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwanyima chakula

Kiongozi wa dhehebu la Good News International, Paul Mackenzie, amepatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwashawishi kufunga hadi kufa katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi.

Hata hivyo, Mahakama Kuu ilimwachilia huru katika mashtaka mengine 115 yaliyohusisha vifo vya waathiriwa wengine, ikisema upande wa mashtaka haukuthibitisha chanzo cha vifo hivyo bila shaka yoyote.

Jaji Alex Ithuku alisema Mackenzie ndiye aliyepanga mpango wa kufunga, akatoa maagizo kuhusu nani angekufa kwanza na kuelekeza wafuasi wake kwenda maeneo yaliyofichwa ili wasifuatiliwe.

Mahakama ilisikiliza ushahidi wa mashahidi waliosema Mackenzie mwenyewe alitangaza maagizo ya kufunga na mpangilio wa vifo. Aliwaambia wafuasi kuwa angekuwa wa mwisho kufa, lakini yeye aliendelea kula huku wengine wakiteseka kwa njaa.

Pia alikataza wafuasi kuomba chakula kutoka kwa majirani. Watoto waliotoroka maeneo ya kufungia walirudishwa kwake, huku mmoja akipigwa kwa kujaribu kutoroka.

Jaji alisema Mackenzie pia aliamuru miili ihamishwe polisi walipokaribia makazi hayo, na alikataa kuruhusu mwili wa mwanamke aliyefariki upelekwe nyumbani kwao kwa mazishi.

Mahakama ilikataa madai kuwa vifo vilitokana na ukame, umaskini au uamuzi wa watu kufunga kwa hiari. Ilibainika kuwa chakula kilikuwepo katika baadhi ya nyumba, huku bwawa la maji likiwa na maji.

“Watu hawafi kwa njaa kando ya bwawa lililojaa maji na ghala lenye chakula kwa bahati mbaya,” alisema Jaji Ithuku.

In brief

Kiongozi wa dhehebu la Good News International, Paul Mackenzie, amepatikana na hatia ya kuua watu 123 kwa kuwashawishi kufunga hadi kufa katika Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi. Ilibainika kuwa chakula kilikuwepo katika baadhi ya nyumba, huku bwawa la maji likiwa na maji. “Watu hawafi kwa njaa kando ya bwawa lililojaa maji na ghala lenye chakula kwa bahati mbaya,” alisema Jaji Ithuku.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.