📰 Newspapers

IEBC yahitaji Sh10bn kununua vifaa vipya vya uchaguzi 2027

IEBC yahitaji Sh10bn kununua vifaa vipya vya uchaguzi 2027

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) huenda ikalazimika kununua vifaa vipya vya teknolojia ya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, hali inayoweza kuongeza mzigo wa matumizi kwa walipa ushuru.

Naibu mwenyekiti wa IEBC Fahima Abdalla aliambia Kamati ya Haki na Masuala ya Sheria ya Bunge la Kitaifa kuwa ukaguzi wa kiufundi uliofanywa na Mamlaka ya ICT (ICTA) ulibaini kuwa vifaa vya usimamizi za uchaguzi Kenya (Kiems) vilivyonunuliwa mwaka 2021 kwa uchaguzi wa 2022 vimefikia mwisho wa muda wake wa matumizi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, vifaa 15,000 vilivyonunuliwa wakati huo haviwezi kutegemewa katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Hali hii ina maana kuwa IEBC italazimika kutafuta angalau Sh10 bilioni kununua vifaa vipya 60,000 ili kuendesha uchaguzi ujao.

“Wataalamu wa Mamlaka ya ICT walikuja kukagua vifaa vya Kiems na kutuambia kuwa teknolojia hiyo ina muda wa matumizi wa miaka mitano. Walitueleza kuwa vifaa hivyo havitafanya kazi ipasavyo katika uchaguzi mkuu wa 2027,” alisema Bi Abdalla.

Kauli yake ilijiri baada ya Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo kutaka kujua ni vifaa vingapi vilivyonunuliwa kwa uchaguzi wa 2022 ambavyo vinaweza kutumika tena mwaka 2027.

Hata hivyo, uamuzi huo unazua wasiwasi kuhusu matumizi ya mabilioni ya fedha za umma kila baada ya miaka mitano, huku serikali ikikabiliwa na mahitaji mengine kama afya, miundombinu na malimbikizo ya madeni.

In brief

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) huenda ikalazimika kununua vifaa vipya vya teknolojia ya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, hali inayoweza kuongeza mzigo wa matumizi kwa walipa ushuru. Hali hii ina maana kuwa IEBC italazimika kutafuta angalau Sh10 bilioni kununua vifaa vipya 60,000 ili kuendesha uchaguzi ujao. Walitueleza kuwa vifaa hivyo havitafanya kazi ipasavyo katika uchaguzi mkuu wa 2027,” alisema Bi Abdalla.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.