📰 Newspapers

Mpango wa TSC kutoa vyeti kwa walimu vya kuendelea kufundisha wazua hisia mseto

Mpango wa TSC kutoa vyeti kwa walimu vya kuendelea kufundisha wazua hisia mseto

PENDEKEZO la Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kuanza kutoa vyeti maalumu kuruhusu walimu kuendelea kufundisha limezua mjadala mkali, huku wadau wa elimu wakitofautiana kuhusu mamlaka ya tume hiyo kusimamia ajira na pia kudhibiti taaluma ya ualimu.

Pendekezo hilo limo katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya TSC wa 2026, unaolenga kufanya mafunzo ya mara kwa mara ya kuwaongezea walimu ujuzi kuwa ya lazima. Walimu watakaokosa kushiriki mafunzo hayo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Hata hivyo, wadau wanatofautiana kuhusu mpango huo. Baadhi wanataka kuundwa kwa chombo huru kitakachosimamia mafunzo na utoaji wa vyeti vya kitaaluma, huku wengine wakitaka serikali ihakikishe walimu hawalazimishwi kulipia mafunzo hayo.

Kifungu cha 28 cha mswada huo kinapendekeza kubadilishwa kwa Kifungu cha 35 cha Sheria ya TSC ili kuipa tume jukumu la kuhakikisha walimu wote wanazingatia viwango vya taaluma ya ualimu.Mswada huo unapendekeza tume iwalazimishe walimu wote waliosajiliwa kushiriki mafunzo ya kuendeleza ujuzi wao na kisha kuwapa vyeti vya kuwaruhusu kuendelea kufundisha.

Mwalimu atakayekosa kutimiza masharti hayo atakabiliwa na hatua za kiutawala zitakazofafanuliwa katika kanuni.Pendekezo hilo lina maana kwamba hata walimu ambao wamesajiliwa na TSC na wamehudumu kwa miaka mingi watalazimika kutimiza masharti mapya ili kupata vyeti hivyo.Ingawa usajili wa TSC unatambua mwalimu kuwa amekidhi masharti ya kujiunga na taaluma, cheti kipya kitategemea ushiriki wake katika mafunzo ya mara kwa mara.

In brief

PENDEKEZO la Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kuanza kutoa vyeti maalumu kuruhusu walimu kuendelea kufundisha limezua mjadala mkali, huku wadau wa elimu wakitofautiana kuhusu mamlaka ya tume hiyo kusimamia ajira na pia kudhibiti taaluma ya ualimu. Walimu watakaokosa kushiriki mafunzo hayo wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Baadhi wanataka kuundwa kwa chombo huru kitakachosimamia mafunzo na utoaji wa vyeti vya kitaaluma, huku wengine wakitaka serikali ihakikishe walimu hawalazimishwi kulipia mafunzo hayo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.