📰 Newspapers

Mke wa Mackenzie alivyosaidia kueneza maovu ya mumewe

Mke wa Mackenzie alivyosaidia kueneza maovu ya mumewe

SIMULIZI ya mauaji ya Shakahola mara nyingi humwangazia kiongozi wa dhehebu la Good News International, Paul Mackenzie, aliyewashawishi mamia ya wafuasi wake kufunga kula hadi kufa wakiamini wangepata wokovu.

Lakini nyuma ya mhubiri huyo aliyekuwa akieneza mafundisho hayo hatari, kulikuwa na mwanamke aliyesaidia kuyadumisha — mkewe, Rhoda Mumbua Maweu.

Mwanzoni mwa uchunguzi, Maweu alionekana kama mwanamke aliyenaswa kwenye mkasa huo kwa sababu tu ya ndoa yake na Mackenzie.

Mahakama hata ilimwachilia kwa dhamana ya Sh300,000, ikisema hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake isipokuwa uhusiano wake na mhubiri huyo.

Hata hivyo, uchunguzi ulipoendelea na mashahidi kueleza maisha ndani ya kanisa hilo, picha tofauti ilianza kujitokeza.

Ushahidi mahakamani ulimuonyesha Maweu kama mtu mwenye ushawishi mkubwa, aliyeshiriki kufundisha na kudhibiti wafuasi.

Alihifadhi vitabu na machapisho ya kidini yaliyotumiwa kuimarisha mafundisho ya kanisa hilo.

Pia alikuwa akiongoza wanawake na watoto, akiwaelekeza kufuata mafundisho ya mumewe.

Mahakama ilimpata na hatia ya kushiriki uhalifu wa kupangwa na kueneza itikadi kali. Ilisema alishiriki shughuli za kundi hilo kwa kuhifadhi machapisho ya kidini na kuwaongoza wanawake na watoto katika masuala ya kiroho.

Hata hivyo, mahakama ilisema upande wa mashtaka haukuwasilisha ushahidi wa kutosha kumhusisha moja kwa moja na utengenezaji au usambazaji wa CD, DVD na vijitabu vilivyopatikana nyumbani kwa Mackenzie.

Ushahidi mwingine uliomhusisha ulitokana na kifo cha Joseph Juma Buyuka akiwa mikononi mwa polisi Watamu.

In brief

SIMULIZI ya mauaji ya Shakahola mara nyingi humwangazia kiongozi wa dhehebu la Good News International, Paul Mackenzie, aliyewashawishi mamia ya wafuasi wake kufunga kula hadi kufa wakiamini wangepata wokovu. Ushahidi mahakamani ulimuonyesha Maweu kama mtu mwenye ushawishi mkubwa, aliyeshiriki kufundisha na kudhibiti wafuasi. Alihifadhi vitabu na machapisho ya kidini yaliyotumiwa kuimarisha mafundisho ya kanisa hilo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.