📰 Newspapers

Gachagua sasa amfunika Uhuru Mlimani wimbi la DCP likizoa wengi

Gachagua sasa amfunika Uhuru Mlimani wimbi la DCP likizoa wengi

CHAMA cha Jubilee kilichomuingiza madarakani Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kilichowahi kutawala siasa za Mlima Kenya, sasa kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Democracy for Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Mei 2025, DCP imevutia viongozi waliokuwa wanachama wa Jubilee, na hivyo kuzidisha vita vya kisiasa kuhusu nani atatawala eneo hilo kuelekea uchaguzi wa 2027.

Baada ya Gachagua kung’olewa mamlakani Oktoba 2024, Jubilee ilianza juhudi za kurejesha ushawishi wake. Uhuru alitangaza kuwa chama hicho kingerejea chini ya uongozi wa Dkt Fred Matiang’i, aliyekuwa akitajwa kuwa mgombeaji wake wa urais.

Lakini Gachagua alipozindua DCP, ushindani wa kisiasa ulizidi. Alisema chama chake ndicho kingekuwa chombo pekee cha kisiasa cha Mlima Kenya, huku vingine vikijivuta.

Miongoni mwa viongozi waliohama kutoka UDA na kujiunga na DCP ni magavana Irungu Kang’ata wa Murang’a na Kiarie Badilisha wa Nyandarua, pamoja na wabunge Wachira Karani, Muchangi Karemba, Rahab Mukami na Martha Wangari.

Aliyekuwa Mbunge wa EALA Kanini Kega, ambaye alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa Uhuru, pia alihamia DCP mwaka 2025. Alisema Jubilee ilikosa uongozi na kwamba wanachama walikuwa wakiondoka kwa wingi.

Huko Nairobi, wabunge wote watatu waliochaguliwa kwa tiketi ya Jubilee—Yusuf Hassan wa Kamukunji, Mark Mwenje wa Embakasi Central na Amos Mwago wa Starehe—wametangaza kuwa watatetea viti vyao kupitia DCP.

In brief

CHAMA cha Jubilee kilichomuingiza madarakani Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na kilichowahi kutawala siasa za Mlima Kenya, sasa kinakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Democracy for Citizens Party (DCP) cha aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Uhuru alitangaza kuwa chama hicho kingerejea chini ya uongozi wa Dkt Fred Matiang’i, aliyekuwa akitajwa kuwa mgombeaji wake wa urais. Lakini Gachagua alipozindua DCP, ushindani wa kisiasa ulizidi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.