KWA miaka mingi Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alikuwa na ushawishi mkubwa katika eneo la Mlima Kenya.
Lakini katika uchaguzi wa 2022 alishuhudia wafuasi wake wengi wwa Mlimani wakipuuza chaguo lake la urithi wa kisiasa, Raila Odinga, wakamuunga mkono aliyekuwa naibu wake, William Ruto.
Sasa, Seneta wa Murang’a Joe Nyutu anasema uamuzi huo haukutokana tu na umaarufu wa Ruto, bali pia makosa ya kisiasa aliyofanya Uhuru katika muhula wake wa pili. Makosa hayo ndiyo yaliumba nafasi kwa naibu wake kujijenga kisiasa neo hilo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo cha redio Jumanne, Nyutu alisema Uhuru alishindwa kudumisha uhusiano wa karibu na viongozi waliochaguliwa Mlima Kenya, na hivyo kumpa Ruto fursa ya kujenga mtandao wake.
“Rais Uhuru Muigai Kenyatta hakuwahi kuwapa viongozi waliochaguliwa Mlima Kenya nafasi ya kukutana naye katika muhula wake wa pili. Unaweza kuthibitisha hilo. Miaka yote mitano,” alisema Nyutu.
Alidai kuwa hata viongozi walipokutana na Uhuru mara nyingi waliondoka wamekerwa na jinsi aliwahudumia.Ruto akatambua pengo hilo na kulitumia kuimarisha uhusiano wake na viongozi na wakazi wa eneo hilo.
“Rais Ruto, ambaye wakati huo alikuwa naibu rais, alitambua kulikuwa na pengo. Viongozi wa Mlima Kenya hawakuwa wakipata nafasi ya kuzungumza na rais (uhuru). Aliona pengo, akalijaza. Aliwakumbatia viongozi hao na alikuwa akipatikana,” akaeleza.
Kauli za Nyutu zinagusia mojawapo ya masuala yaliyotikisa Jubilee katika muhula wa pili wa Uhuru: uhusiano uliokuwa ukizorota…