📰 Newspapers

Mzozo wa ardhi ya Mau warejea Gideon Moi akilaumu serikali

Mzozo wa ardhi ya Mau warejea Gideon Moi akilaumu serikali

MZOZO kuhusu umiliki wa ardhi inayozunguka Msitu wa Mau umekuwa zaidi ya suala la uhifadhi wa mazingira.

Kwa miaka mingi, umekuwa chanzo cha migawanyiko ya kisiasa, kuvunjika kwa urafiki na kubadilisha miungano ya uchaguzi katika eneo la Bonde la Ufa.

Sasa, huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi ameibua tena suala hilo, akionya kuwa Kenya inaweza kuingia katika uchaguzi mwingine bila kutatua dhuluma za kihistoria zilizokumba maelfu ya familia zilizofurushwa.

Akizungumza nyumbani kwake Kabarak alipokutana na ujumbe kutoka Ololung’a, Kaunti ya Narok, Bw Moi alihoji ikiwa serikali inaweza kuomba muhula mwingine bila kutoa suluhu kwa wakazi hao.

“Tusipotatua suala la Mau katika utawala huu, tukiingia katika uchaguzi mwingine, je, suala hili litawahi kutatuliwa?” aliuliza.

Mzozo huo ulizua mgawanyiko mkubwa katika serikali ya muungano ya Rais Mwai Kibaki na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga wakati wa operesheni za kufurusha wakazi msituni mwaka 2008 na 2009.

Serikali ilikabiliwa na changamoto ya kusawazisha uhifadhi wa mojawapo ya vyanzo muhimu vya maji nchini na madai ya familia zilizosema zilinunua au kupewa ardhi kihalali.

Ripoti ya Tume ya Ndung’u ya mwaka 2004 ilifichua ugawaji wa ardhi uliotiliwa shaka katika mfumo wa ikolojia wa Mau na kupendekeza kufutwa kwa hati zilizotolewa kinyume cha sheria.

Mnamo Julai 2008, Raila alianzisha mpango wa kurejesha msitu, huku jopo kazi likipewa jukumu la kupendekeza namna ya kuwahamisha…

In brief

MZOZO kuhusu umiliki wa ardhi inayozunguka Msitu wa Mau umekuwa zaidi ya suala la uhifadhi wa mazingira. Sasa, huku uchaguzi wa 2027 ukikaribia, mwenyekiti wa Kanu Gideon Moi ameibua tena suala hilo, akionya kuwa Kenya inaweza kuingia katika uchaguzi mwingine bila kutatua dhuluma za kihistoria zilizokumba maelfu ya familia zilizofurushwa. “Tusipotatua suala la Mau katika utawala huu, tukiingia katika uchaguzi mwingine, je, suala hili litawahi kutatuliwa?” aliuliza.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.