📰 Newspapers

SHERIA: Ndoa ya wengi hubadilishwa kwa hiari ya wanandoa kuwa ya mke mmoja

SHERIA: Ndoa ya wengi hubadilishwa kwa hiari ya wanandoa kuwa ya mke mmoja

WANANDOA wana uhuru wa kubadilisha aina ya ndoa yao kutoka ile inayoweza kuwa ya wake wengi na kuwa ya mke mmoja, lakini sheria inataka uamuzi huo ufanywe kwa hiari na kwa makubaliano ya wote wawili.

Kifungu cha nane kuhusu ubadilishaji wa ndoa kinaeleza kuwa wanandoa wanaweza kutangaza rasmi nia yao ya kubadili ndoa yao na kuifanya iwe ya mke mmoja badala ya ile inayoweza kuwa ya wake wengi.

Hata hivyo, sheria inaweka masharti maalumu kwa wanandoa wanaotaka kufanya mabadiliko hayo. Kwanza, kila mmoja lazima akubali kwa hiari bila kulazimishwa na mwenzake. Hii ina maana kuwa mume au mke hawezi kufanya uamuzi huo peke yake bila kupata ridhaa ya mwenzake.

Kwa upande wa ndoa ambayo tayari ina wake wengi, sheria inaweka kizuizi zaidi. Ndoa ya aina hiyo haiwezi kubadilishwa kuwa ya mke mmoja ikiwa mume ana zaidi ya mke mmoja wakati wa kutaka kufanya mabadiliko hayo.

Hivyo, mume mwenye wake wawili au zaidi hawezi kutumia utaratibu huu kubadilisha ndoa yake kuwa ya mke mmoja. Sharti hilo linaonyesha kuwa sheria inatambua tofauti kati ya ndoa inayoweza kuwa ya wake wengi na ile ambayo tayari ina wake wengi.

Ili mabadiliko hayo yatambulike rasmi, wanandoa wanapaswa kutoa tangazo lao mbele ya afisa wa ndoa. Tangazo hilo lazima liandikwe na kutiwa saini na kila mmoja wao kuthibitisha kuwa wamekubaliana kufanya mabadiliko hayo.

In brief

WANANDOA wana uhuru wa kubadilisha aina ya ndoa yao kutoka ile inayoweza kuwa ya wake wengi na kuwa ya mke mmoja, lakini sheria inataka uamuzi huo ufanywe kwa hiari na kwa makubaliano ya wote wawili. Sharti hilo linaonyesha kuwa sheria inatambua tofauti kati ya ndoa inayoweza kuwa ya wake wengi na ile ambayo tayari ina wake wengi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.