📰 Newspapers

Mwanahabari kulipwa fidia Sh1.5 milioni kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano

Mwanahabari kulipwa fidia Sh1.5 milioni kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano

MWANAHABARI wa kampuni ya MediaMax Catherine Wanjeri Kariuki amezawidiwa fidia ya Sh1.5 milioni na mahakama baada ya polisi kumpiga risasi mguuni alipokuwa akiripoti maandamano ya Julai 16, 2024.

Bi Wanjeri alipigwa risasi tatu za mpira zilizofyatuliwa na polisi katika barabara ya Kenyatta jijini Nakuru alipokuwa akiripoti maandamano ya vijana kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Katika uamuzi wake, mahakama ilisema kitendo cha polisi kumpiga risasi mwandishi huyo alipokuwa akitekeleza wajibu wake kilikiuka haki zake za kikatiba, za utu, usalama wa kibinafsi, uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Mahakama iliamuru serikali kumlipa fidia ya jumla ya Sh1.5 milioni pamoja na riba kuanzia tarehe ya kutolewa kwa hukumu hadi atakapolipwa kikamilifu.

Aidha, mahakama ilitangaza kuwa kuwapiga risasi, kuwashambulia, kuwanyanyasa, kuwakamata kiholela au kuwatisha wanahabari walioidhinishwa kuripoti maandamano ni kinyume cha Katiba.

Mahakama pia iliagiza Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi (IPOA) kukamilisha ndani ya siku 90 uchunguzi wake kuhusu mashambulizi dhidi ya wanahabari wakati wa maandamano ya Juni na Julai 2024, hususan tukio la Bi Wanjeri, na kuwasilisha ripoti kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP).

Kesi hiyo iliwasilishwa mnamo 2024 na Muungano wa Wanahabari Kenya (KUJ), Chama cha Wahariri Kenya na kitengo cha Independent Medico-Legal Unit (IMLU) kupinga ukiukaji wa haki za wanahabari.

In brief

MWANAHABARI wa kampuni ya MediaMax Catherine Wanjeri Kariuki amezawidiwa fidia ya Sh1.5 milioni na mahakama baada ya polisi kumpiga risasi mguuni alipokuwa akiripoti maandamano ya Julai 16, 2024. Bi Wanjeri alipigwa risasi tatu za mpira zilizofyatuliwa na polisi katika barabara ya Kenyatta jijini Nakuru alipokuwa akiripoti maandamano ya vijana kupinga Mswada wa Fedha wa 2024. Aidha, mahakama ilitangaza kuwa kuwapiga risasi, kuwashambulia, kuwanyanyasa, kuwakamata kiholela au kuwatisha wanahabari walioidhinishwa kuripoti maandamano ni kinyume cha Katiba.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.