📰 Newspapers

Hii kazi ni ngumu kuliko vile nilitarajia, akiri kocha Pochettino kuhusu Man United

Hii kazi ni ngumu kuliko vile nilitarajia, akiri kocha Pochettino kuhusu Man United

MANCHESTER, Uingereza: KOCHA mkuu wa Manchester United, Mauricio Pochettino, amekiri kuwa kazi ya kuinoa timu hiyo ni “ngumu zaidi kuliko alivyotarajia” kufuatia kichapo cha 4-0 kutoka kwa Brentford katika Ligi Kuu Uingereza (EPL). Matokeo hayo yameifanya United kupoteza mechi mbili mfululizo kwa tofauti ya mabao manne, baada ya awali kufungwa 4-0 na Liverpool, huku timu hiyo ikishuka hadi nafasi ya 19 kwenye…

MANCHESTER, Uingereza:

KOCHA mkuu wa Manchester United, Mauricio Pochettino, amekiri kuwa kazi ya kuinoa timu hiyo ni “ngumu zaidi kuliko alivyotarajia” kufuatia kichapo cha 4-0 kutoka kwa Brentford katika Ligi Kuu Uingereza (EPL).

Matokeo hayo yameifanya United kupoteza mechi mbili mfululizo kwa tofauti ya mabao manne, baada ya awali kufungwa 4-0 na Liverpool, huku timu hiyo ikishuka hadi nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Pochettino alikiri ukubwa wa changamoto inayomkabili, akisema:

“Bila shaka, ndiyo. Kazi hii ni ngumu zaidi kuliko nilivyotarajia.”

Aliongeza kuwa kikosi chake kinahitaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutambua makosa na kutafuta jinsi ya kuboresha kiwango chake.

“Tulipofungwa bao la kwanza kutokana na shuti la kwanza lililolenga lango, ilikuwa vigumu kwa wachezaji kurejea mchezoni. Tulifungwa mabao manne kutokana na mashuti manne yaliyolenga lango. Matokeo haya yanaumiza sana,” alisema Pochettino.

Kocha huyo amesisitiza kuwa tatizo kubwa la United kwa sasa ni kukosa mwendelezo wa kiwango kizuri.

“Wakati mwingine tunaonesha ubora kwa dakika 20 pekee. Tunahitaji kuwa na kiwango kizuri kwa muda wote wa mchezo.”

Pamoja na matokeo hayo mabaya, Pochettino amewataka wachezaji wake wasikate tamaa, akisisitiza kuwa ataendelea kupambana kuboresha timu.

“Siwezi kuacha kufanya kazi. Wachezaji wanapaswa kuamini kuwa tunaweza kufanya vizuri zaidi. Ni lazima tujifunze kutokana na maumivu haya na kuwa bora kutoka hapa,” aliongezea.

In brief

MANCHESTER, Uingereza: KOCHA mkuu wa Manchester United, Mauricio Pochettino, amekiri kuwa kazi ya kuinoa timu hiyo ni “ngumu zaidi kuliko alivyotarajia” kufuatia kichapo cha 4-0 kutoka kwa Brentford katika Ligi Kuu Uingereza (EPL). Kazi hii ni ngumu zaidi kuliko nilivyotarajia. Pamoja na matokeo hayo mabaya, Pochettino amewataka wachezaji wake wasikate tamaa, akisisitiza kuwa ataendelea kupambana kuboresha timu.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.