Zipo sababu tele za kuamini uajiri wa walimu unafanywa kwa upendeleo

Zipo sababu tele za kuamini uajiri wa walimu unafanywa kwa upendeleo

YAPO maswali halali kuhusu uwazi na usawa katika uajiri wa walimu nchini.

Walimu waliohitimu, wenye uzoefu na walio na umri wa zaidi ya miaka 40 wameendelea kusubiri ajira kwa miaka mingi, huku Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) ikiendelea kuajiri maelfu ya walimu wapya.

Hali hii inahitaji maelezo ya kuridhisha. Haiingii akilini kwamba mtu aliyesomea ualimu, akafaulu mafunzo yake na akatumia miaka mingi kusubiri ajira, anaweza kutupiliwa mbali kwa mwaka baada ya mwaka.

Tume ina wajibu wa kueleza kwa nini walimu wenye umri mkubwa wameachwa nyuma.

Ikiwa kuna sera inayowapa vijana kipaumbele, ni lazima iwekwe wazi na ijadiliwe kwa misingi ya haki. Walimu hawa hawakuchagua kusubiri ajira kwa miongo kadhaa.

Wengi wanaishi kwa vibarua na mishahara duni katika shule za kibinafsi huku wakitumai siku moja kupata nafasi serikalini.

Hali hii inazua pia tuhuma nzito kwamba nafasi za ajira zinaweza kuwa zinagawa kwa upendeleo wa kisiasa.

Kuna madai kuwa barua za ajira zinaweza kuuzwa au kutolewa kwa watu wenye uhusiano na wanasiasa wanaounga mkono serikali.

Haya ni madai yanayohitaji kuchunguzwa, si kuachwa yaendelee kama uvumi. TSC inapaswa kuweka wazi vigezo, orodha za waliofaulu na sababu za walioachwa baada ya uajiri.

Ikiwa ajira zinatolewa kwa misingi ya uaminifu wa kisiasa, basi mfumo mzima wa elimu unakuwa mateka wa siasa.

In brief

YAPO maswali halali kuhusu uwazi na usawa katika uajiri wa walimu nchini. Walimu waliohitimu, wenye uzoefu na walio na umri wa zaidi ya miaka 40 wameendelea kusubiri ajira kwa miaka mingi, huku Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) ikiendelea kuajiri maelfu ya walimu wapya. Tume ina wajibu wa kueleza kwa nini walimu wenye umri mkubwa wameachwa nyuma. Walimu hawa hawakuchagua kusubiri ajira kwa miongo kadhaa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics

Help us understand visits and countries – anonymous and aggregated.

Marketing

Used to measure and personalise adverts and social media content.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.