📰 Newspapers

Maaskofu wa kanisa Katoliki wakemea wanasiasa wanaorushiana matusi

Maaskofu wa kanisa Katoliki wakemea wanasiasa wanaorushiana matusi

MAASKOFU wa Kanisa Katoliki wamewakosoa wagombeaji wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2027 kwa kutumia matamshi ya kikabila, matusi na uchochezi, wakionya kuwa lugha hiyo inaweza kuzua machafuko nchini.

Viongozi hao wa kanisa walisema wanasiasa wanapaswa kuzingatia athari za kauli zao kwa taifa, hasa wakati huu ambapo joto la kisiasa linaanza kupanda kuelekea uchaguzi mkuu.Katika taarifa iliyotolewa jana katika Kituo cha John Cardinal Njue Pastoral Centre, Embu, waliwataka wagombeaji na wafuasi wao kuwa waangalifu wanapozungumza hadharani na kuepuka lugha inayodhalilisha wapinzani.

Taarifa hiyo ilisomwa na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (KCCB), Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba, akiwa pamoja na naibu wake, Askofu Mkuu Anthony Muheria.“Tunawakumbusha wanasiasa kuwa kampeni kali hazipaswi kuwa kisingizio cha kutumia lugha inayogawanya wananchi. Maneno ya chuki yanaweza kuharibu amani tuliyo nayo,” walisema.

Katika siku za hivi majuzi, Rais William Ruto, aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wamekuwa wakirushiana vijembe, huku baadhi ya kauli zao zikionekana kulenga watu binafsi badala ya kujadili sera na masuala yanayowakabili Wakenya.

Maaskofu walisema matumizi ya matusi na lugha ya kudhalilisha yanatoa mfano mbaya kwa watoto na vijana wanaotazama viongozi kama vielelezo vya tabia njema.

Walisema pia kuwa ingawa kipindi rasmi cha kampeni bado hakijaanza, wanaotafuta nyadhifa za kisiasa wanapaswa kuonyesha ustaarabu katika maneno na mienendo yao.Walitoa wito kwa wagombeaji wote wa urais kutoa ahadi hadharani…

In brief

MAASKOFU wa Kanisa Katoliki wamewakosoa wagombeaji wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2027 kwa kutumia matamshi ya kikabila, matusi na uchochezi, wakionya kuwa lugha hiyo inaweza kuzua machafuko nchini. Taarifa hiyo ilisomwa na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (KCCB), Askofu Mkuu Maurice Muhatia Makumba, akiwa pamoja na naibu wake, Askofu Mkuu Anthony Muheria.“Tunawakumbusha wanasiasa kuwa kampeni kali hazipaswi kuwa kisingizio cha kutumia lugha inayogawanya wananchi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.