📰 Newspapers

Kinachowakosesha usingizi vinara wa upinzani wakikabili Ruto 2027

Kinachowakosesha usingizi vinara wa upinzani wakikabili Ruto 2027

Viongozi wa upinzani nchini wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kisiasa wanapojaribu kuungana kumng’oa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Licha ya matamshi ya kutaka umoja na mazungumzo kuhusu kumpata mgombea mmoja wa urais, viongozi hao wanahangaishwa na maswali kuhusu nani atapewa tiketi, nani atajiondoa na jinsi watakavyogawana mamlaka iwapo watashinda.

Kalonzo Musyoka, Edwin Sifuna, Rigathi Gachagua, Fred Matiang’i na Martha Karua ni miongoni mwa viongozi wanaokabiliwa na changamoto hizo. Kwa baadhi yao, uchaguzi ujao unaweza kuwa nafasi ya mwisho kutimiza ndoto ya kuingia Ikulu, huku wengine wakihofia kupoteza ushawishi wa kisiasa au kusahaulika iwapo muungano utashindwa.

Utafiti wa kampuni ya TIFA uliotolewa Alhamisi umeongeza presha katika mazungumzo hayo. Asilimia 43 ya waliohojiwa wanamtaja Gachagua kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa umoja wa upinzani. Rais Ruto anafuata kwa asilimia 15, Sifuna asilimia saba na Kalonzo asilimia sita.

Dkt Matiang’i na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kila mmoja alipata asilimia nne, huku Rais mstaafu Uhuru Kenyatta akipata asilimia mbili.

Hata hivyo, mgogoro wa uongozi umeanza kujitokeza ndani ya vuguvugu la Linda Mwananchi, baada ya Babu kufichua kuwa kulikuwa na makubaliano ya awali kuhusu jinsi yeye na Sifuna wangeshirikiana kisiasa.

Alisema walikuwa wamekubaliana Sifuna awe mgombea urais huku yeye akiongoza chama kipya, lakini mpango huo ulibadilika.

In brief

Viongozi wa upinzani nchini wanakabiliwa na mtihani mgumu wa kisiasa wanapojaribu kuungana kumng’oa Rais William Ruto madarakani katika uchaguzi mkuu wa 2027. Asilimia 43 ya waliohojiwa wanamtaja Gachagua kuwa kikwazo kikubwa zaidi kwa umoja wa upinzani. Rais Ruto anafuata kwa asilimia 15, Sifuna asilimia saba na Kalonzo asilimia sita. Dkt Matiang’i na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino kila mmoja alipata asilimia nne, huku Rais mstaafu Uhuru Kenyatta akipata asilimia mbili.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.