📰 Newspapers

Uchovu, mwendo wa kasi wahatarisha madereva katika barabara ya Mombasa-Malaba

Uchovu, mwendo wa kasi wahatarisha madereva katika barabara ya Mombasa-Malaba

Uchovu wa madereva, mwendo wa kasi na matumizi ya vileo na dawa za kulevya vinahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara kuu ya Mombasa-Malaba, ambako zaidi ya maeneo 200 yametambuliwa kuwa hatari kwa ajali.

Wadau wa sekta ya uchukuzi wanasema kuongezeka kwa malori yanayosafirisha bidhaa katika barabara hiyo, pamoja na msongamano na miundombinu duni, kunazidisha hatari ya ajali.

Wito huo umetolewa Kenya ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waathiriwa wa Ajali za Barabarani kesho, Novemba 15, kwa kaulimbiu, “Wekeza katika Usalama, Sio Mwendo Kasi”.

Takwimu za Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) zinaonyesha watu 5,009 walifariki katika ajali mwaka 2025, ikilinganishwa na 4,748 mwaka 2024, ongezeko la asilimia 5.5.

Ajali zilizoripotiwa ziliongezeka kutoka 11,165 hadi 11,638, huku idadi ya waliojeruhiwa ikipanda kutoka 24,245 hadi 24,905.

Afisa wa Polisi anayesimamia Ukanda wa Kaskazini, Beatrice Kiraguri, alisema makosa ya madereva, uchovu na matumizi ya vileo ni miongoni mwa sababu kuu za ajali.

Akizungumza wakati wa kampeni ya siku tano iliyoanzia Mombasa na kuhitimishwa Malaba Ijumaa, aliwataka madereva wa malori, magari ya umma, waendesha bodaboda na watembea kwa miguu kuwajibika.

Kampeni hiyo inaongozwa na Mamlaka ya Uratibu wa Usafiri na Biashara ya Ukanda wa Kaskazini (NCTTCA), kwa ushirikiano na NTSA, KeNHA, polisi na Chama cha Wasafirishaji Kenya.

In brief

Uchovu wa madereva, mwendo wa kasi na matumizi ya vileo na dawa za kulevya vinahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara kuu ya Mombasa-Malaba, ambako zaidi ya maeneo 200 yametambuliwa kuwa hatari kwa ajali. Wadau wa sekta ya uchukuzi wanasema kuongezeka kwa malori yanayosafirisha bidhaa katika barabara hiyo, pamoja na msongamano na miundombinu duni, kunazidisha hatari ya ajali.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.