Washirika wa Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya wameanzisha mkakati mpya wa kisiasa unaolenga kumrejeshea angalau asilimia 40 ya kura za eneo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, licha ya kuongezeka kwa ushawishi wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Mpango huo unaoitwa Diehard Movement unaongozwa na Mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri na mwenzake wa Ndia, George Kariuki. Unalenga kujenga mtandao wa wafuasi wa Ruto katika ngazi za mashinani badala ya kutegemea mikutano mikubwa ya kisiasa.
Kiunjuri alisema lengo lao ni kuthibitisha kuwa bado kuna wakazi wa Mlima Kenya wanaomuunga mkono Rais na walio tayari kufanya kampeni kuhakikisha anapata angalau asilimia 40 ya kura za eneo hilo.
Alisema harakati hizo zitajikita katika kaunti za Meru, Tharaka Nithi, Embu, Nyeri, Murang’a, Kirinyaga, Nyandarua, Laikipia, Nakuru, Nairobi, Kiambu na Lamu.
Mpango huo unajumuisha mikutano ya wananchi, mashindano ya kandanda kwa vijana na kuunda mitandao ya viongozi wa mashinani watakaohamasisha wapiga kura.
Kariuki alisema washirika hao hawana muda wa kukaa kwenye mikutano ya ndani, bali wanataka kuzungumza moja kwa moja na wananchi na kuwaeleza kuhusu miradi ya maendeleo ya serikali, hasa barabara.
Hata hivyo, alikiri kuwa bado hawajafikia kiwango wanachotaka, akisema serikali imekosa kiongozi mwenye ushawishi wa kuwaunganisha viongozi wa eneo hilo tangu Gachagua alipoondolewa mamlakani.
Harakati hizo zinajitokeza huku Gachagua na rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakionekana kuwa na ushawishi mkubwa…