BRAGA, Ureno:
URENO ilianza maisha bila nahodha wake Cristiano Ronaldo kwa kichapo kizito cha 4-1 dhidi ya Denmark kwenye Uwanja wa Braga, katika mechi ya Mataifa ya Ulaya Jumamosi usiku.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza tangu mshambuliaji huyo kutangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Ronaldo, 41, alitangaza kustaafu kwake wiki jana kupitia video aliyoweka kwenye mitandao ya kijamii, akisitisha safari ndefu iliyoanza mwaka 2003.
Katika kipindi hicho, aliandikisha rekodi za dunia kwa kufunga mabao 146 na kucheza mechi 234, pamoja na kunyakua tuzo ya Ballon d'Or mara tano.
Licha ya uamuzi huo, kocha Jorge Jesus alisema baadaye kuwa Ronaldo angeitwa kwenye kikosi cha Ligi ya Mataifa ya Ulaya dhidi ya Denmark na Wales.
Ikumbukwe, fowadi huyo aliondoka kambini mwezi Septemba baada ya kuambiwa hataanza mchezo wa kwanza dhidi ya Denmark, hatua iliyomgharimu faini pauni 255 (Sh45,000) na marufuku ya siku 30.
Mechi ya Jumamosi iligeuka sherehe za kumuaga shujaa wao. Wachezaji na watoto walioandamana nao waliingia uwanjani wakiwa wamevalia jezi iliyoandikwa 'Ronaldo 7', huku mashabiki wakibandika bango kubwa lililoandikwa 'Ronaldo' kwenye ghorofa ya juu na 'GOAT' chini yake.
Bango jingine lilisomeka 'Asante, Nahodha', ujumbe ambao pia ulionekana kwenye ubao wa matokeo dakika ya saba.
Hata hivyo, sherehe hizo ziliharibiwa na Denmark.
Kiungo wa zamani wa Southampton na Tottenham, Pierre-Emile Hojbjerg, aliifungia Denmark kwa penalti dakika chache kabla ya mapumziko baada…