📰 Newspapers

Papa Leo XIV aunda jimbo kuu jipya la Eldoret, ateua Obanyi kuwa askofu mkuu

Papa Leo XIV aunda jimbo kuu jipya la Eldoret, ateua Obanyi kuwa askofu mkuu

KIONGOZI wa kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Leo XIV, ameunda Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Eldoret na kumteua Askofu Joseph Obanyi Sagwe wa Kakamega kuwa askofu mkuu wa kwanza wa dayosisi hiyo mpya.

Tangazo hilo lilitolewa Ijumaa saa nane mchana saa za Kenya kupitia taarifa rasmi iliyotumwa kwa maaskofu nchini na ofisi ya Mwakilishi wa Papa nchini Kenya.

Jimbo Kuu la Eldoret litakuwa na dayosisi nne: Lodwar, Kapsabet, Kitale na Kericho.

Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa katika muundo wa kanisa Katoliki nchini, hasa maeneo ya Magharibi na Kaskazini-Magharibi ambako kanisa limekuwa likipanua shughuli zake na huduma kwa waumini.

Askofu Obanyi amekuwa akiongoza dayosisi ya Eldoret kwa muda kama msimamizi baada ya Askofu Mkuu Dominic Kimengich kuhamishiwa Mombasa kuwa askofu mkuu msaidizi.

Katika wadhifa wake mpya Obanyi ataongoza Jimbo Kuu la Eldoret na kuimarisha ushirikiano kati ya dayosisi nne zilizo chini yake.

Dayosisi za Lodwar, Kapsabet na Kitale awali zilikuwa chini ya Jimbo Kuu la Kisumu, huku Kericho ikiwa chini ya Jimbo Kuu la Nairobi.

Kuanzishwa kwa Jimbo Kuu la Eldoret kunalenga kurahisisha uratibu wa shughuli za kanisa na kuimarisha huduma kwa waumini katika eneo hilo.

Obanyi alizaliwa mwaka 1967 katika eneo la Kebiro, Dayosisi ya Kisii.

Alisomea falsafa katika Seminari Kuu ya St Augustine, Mabanga, kabla kuendelea na masomo ya theolojia katika Seminari Kuu ya St Thomas Aquinas jijini Nairobi.

In brief

KIONGOZI wa kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Leo XIV, ameunda Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Eldoret na kumteua Askofu Joseph Obanyi Sagwe wa Kakamega kuwa askofu mkuu wa kwanza wa dayosisi hiyo mpya. Askofu Obanyi amekuwa akiongoza dayosisi ya Eldoret kwa muda kama msimamizi baada ya Askofu Mkuu Dominic Kimengich kuhamishiwa Mombasa kuwa askofu mkuu msaidizi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.