📰 Newspapers

Papa Leo XIV akataa ombi la mapadri la kuoa

Papa Leo XIV akataa ombi la mapadri la kuoa

ROMA, Italia: KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, amesema hana mpango wa kubadilisha mafundisho ya kanisa hilo ili kuruhusu mapadri kufunga ndoa, akionya kuwa suala hilo linaweza kuzua migawanyiko miongoni mwa waumini wake wapatao bilioni 1.4. Katika matamshi yake ya kwanza kuhusu pendekezo hilo linaloungwa mkono na baadhi ya Wakatoliki, Papa Leo alisema kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha umoja…

ROMA, Italia:

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, amesema hana mpango wa kubadilisha mafundisho ya kanisa hilo ili kuruhusu mapadri kufunga ndoa, akionya kuwa suala hilo linaweza kuzua migawanyiko miongoni mwa waumini wake wapatao bilioni 1.4.

Katika matamshi yake ya kwanza kuhusu pendekezo hilo linaloungwa mkono na baadhi ya Wakatoliki, Papa Leo alisema kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha umoja katika kanisa hilo duniani.

Hata hivyo, hakufunga mlango kabisa kwa uwezekano wa mabadiliko hayo siku zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege iliyokuwa ikimrejesha Roma baada ya ziara ya siku 12 Amerika Kusini, Papa Leo alisema kuruhusu mapadri waliofunga ndoa kuhudumu kunaweza kusababisha migawanyiko katika baadhi ya maeneo ya kanisa.

"Huenda baadhi ya mambo yakabadilika siku zijazo. Hata hivyo, kwa sasa ninaamini sehemu muhimu ya huduma yangu kanisani ni kuponya roho na kuwaunganisha watu," akasema.

Aliongeza kuwa anataka kuwapa Wakatoliki muda wa kutathmini masuala yanayostahili kupewa kipaumbele na kanisa na kuamua namna bora ya kukabiliana nayo.

"Ninafahamu vyema kuwa watu wengi hawakubaliani na msimamo huo. Hilo si tatizo. Suala zima la wanaume waliofunga ndoa kuhudumu kama mapadri ni tata," akasema.

Mapadri wengi wa Kanisa Katoliki huapa kutofunga ndoa na kujitolea kikamilifu kwa huduma ya kanisa.

Wanaounga mkono kuruhusu mapadri kufunga ndoa wanasema hatua hiyo inaweza kuwavutia wanaume wengi zaidi kujiunga na huduma ya upadri, hivyo kupunguza uhaba…

In brief

ROMA, Italia: KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, amesema hana mpango wa kubadilisha mafundisho ya kanisa hilo ili kuruhusu mapadri kufunga ndoa, akionya kuwa suala hilo linaweza kuzua migawanyiko miongoni mwa waumini wake wapatao bilioni 1.4. Suala zima la wanaume waliofunga ndoa kuhudumu kama mapadri ni tata," akasema. Mapadri wengi wa Kanisa Katoliki huapa kutofunga ndoa na kujitolea kikamilifu kwa huduma ya kanisa.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.