PETER Nyang’au atakapojiunga na Gredi 10 Januari 2027, atakuwa tayari amepiga hatua kutokana na mradi wake wa ufugaji sungura alioanzisha miaka miwili iliyopita.
Peter anasimulia kuchochewa na rafiki yake mnamo 2025, aliyefuga sungura nyumbani kwao eneo la Elburgon, Kaunti ya Nakuru.
"Nilikuwa nikimtembelea radfiki yangu mara kwa mara na kwa wakati mwingine nilimsaidia kuchinja sungura mmoja. Siku moja, mama yake aliniambia kuwa ufugaji wa sungura ni mzuri, kwani unaweza kunisaidia kukidhi mahitaji yangu binafsi bila kutegemea sana wazazi wangu," anakumbuka Peter na kuongeza kuwa mzazi huyo aliahidi kumuuzia sungura wawili iwapo angekuwa tayari kuanzisha mradi huo.
Peter alipowasilisha wazo hilo kwa wazazi wake, walifurahi sana na kukubali kumuunga mkono.
Kwa mtaji wa Sh500, mwanafunzi huyo alinunua sungura wawili wa wastani, dume na jike kwa Sh150 kila mmoja.
Kwa fedha zilizobaki alizitumia kununua misumari, mbao na vifaa vingine vya kujengea banda la muda kwa ajili ya mradi wake mpya.
Wakati wa wikendi, alitafuta chakula cha kutosha kutoka kwa maeneo ya shamba yasiyolimwa, huku akimwachia baba yake jukumu la kuwalisha na kuwatunza, hasa wakati alipokuwa shuleni.
Katika ziara ya hivi majuzi nyumbani kwa wazazi wake katika eneo la Turi Farmers mjini Elburgon, Kaunti ya Nakuru, Peter,15 alieleza kuwa baada ya miezi michache sungura alizaa wana 12.
Anasema kuwa kuzaliwa kwa kundi hilo kulikuwa mwanzo wa ufanisi wa ufugaji wake, jambo lililomfanya aongeze…