📰 Newspapers

Mafuriko yaangamiza 6, zaidi ya 600 wafurushwa makwao mvua ikiendelea kunyesha

Mafuriko yaangamiza 6, zaidi ya 600 wafurushwa makwao mvua ikiendelea kunyesha

TAKRIBAN familia 603 zimefurushwa makwao na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku watu sita wakipoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayonyesha wakati huu wa msimu wa mvua wa Oktoba, Novemba na Desemba.

Ripoti ya Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya inaonyesha kuwa jumla ya familia 1,141 zimeathiriwa na mafuriko, huku maji yakiharibu nyumba, mashamba, kukatiza barabara na kuhatarisha maisha ya wakazi wanaoishi karibu na mito na maeneo ya mabonde.

Kaunti za Tana River na Taita-Taveta ndizo zilizoathirika zaidi. Tana River imerekodi idadi kubwa zaidi ya familia zilizoathirika, huku familia 796 zikikumbwa na mafuriko na 525 zikilazimika kuhama makazi yao.

Katika Kaunti ya Taita-Taveta, familia kadhaa zimeachwa bila makazi baada ya mito kufurika katika mji wa Voi Jumatatu, na maji kuingia katika maeneo ya makazi.

Hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kadri msimu wa mvua unavyozidi kushika kasi.

Idara ya Hali ya Hewa imetabiri kuwa mvua itaendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini kati ya Novemba 17 na 23.

Watu sita wamefariki katika matukio tofauti. Watoto wawili walisombwa na maji ya mafuriko ya ghafla katika Kaunti ya Kajiado, huku wengine wawili wakizama Turkana.

Watu wengine wawili walifariki baada ya mashua kupinduka katika Kaunti ya Kitui, huku abiria wawili wakiendelea kutafutwa.

Katika Kaunti ya Tana River, maeneo ya Tana Kaskazini yameathirika zaidi baada ya maji ya Laga Wardesa kufurika na kuingia katika…

In brief

TAKRIBAN familia 603 zimefurushwa makwao na mafuriko yanayoendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini, huku watu sita wakipoteza maisha kutokana na mvua kubwa inayonyesha wakati huu wa msimu wa mvua wa Oktoba, Novemba na Desemba. Katika Kaunti ya Tana River, maeneo ya Tana Kaskazini yameathirika zaidi baada ya maji ya Laga Wardesa kufurika na kuingia katika…

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.