📰 Newspapers

Wasiwasi idadi ya viboko waliokufa Ziwa Naivasha ikipanda

Wasiwasi idadi ya viboko waliokufa Ziwa Naivasha ikipanda

WAVUVI katika Ziwa Naivasha wameingiwa na hofu baada ya viboko wengine watatu kupatikana wamekufa majini, na kufikisha tisa idadi ya wanyama hao waliofariki katika kipindi cha wiki tatu.

Mwanachama wa Kamere Beach Management Unit (BMU), Bw Labaan Ewoi, alisema viboko wawili walipatikana katika maeneo ya Malewa na Crayfish Jumatano, huku mwingine akionekana katika eneo la Fishermen Alhamisi asubuhi.

Alisema wavuvi wenzake walimuarifu baada ya kuona mizoga hiyo ikielea majini walipokuwa wakielekea kazini.

Bw Ewoi, ambaye amekuwa mvuvi kwa miaka tisa, alisema wakazi wana wasiwasi kwa kuwa Shirika la Kulinda Wanyama Pori Kenya (KWS) lilikuwa limeahidi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha vifo hivyo, lakini visa vinaendelea kuripotiwa.

“Maafisa wa KWS walipokuja walisema watafanya uchunguzi kwa sababu vifo hivyo vimekuwa vingi na walihitaji kubaini chanzo chake. Tunahofia hali hii kwa sababu si kawaida kusikia visa kama hivi Naivasha. Viboko hulisha katika maeneo ya kandokando ya ziwa,” alisema.

Bw Ewoi alisema Novemba 12, 2026, aliona viboko wawili wakielea majini katika eneo la Kibokoni na akatuma picha kwa KWS.

Baadaye, wavuvi wengine waliripoti mizoga miwili katika eneo la Malewa, ambayo ilikuwa imevimba.

Baadhi ya mizoga haikuwa na majeraha yanayoonekana, huku mmoja ukiwa tayari umeanza kuoza.

KWS imethibitisha kupata mizoga mitano, huku kifo kingine kikiwa bado hakijathibitishwa.

Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Mawasiliano wa shirika hilo, Bw Duncan Juma, alisema maafisa wa wanyamapori…

In brief

WAVUVI katika Ziwa Naivasha wameingiwa na hofu baada ya viboko wengine watatu kupatikana wamekufa majini, na kufikisha tisa idadi ya wanyama hao waliofariki katika kipindi cha wiki tatu. Alisema wavuvi wenzake walimuarifu baada ya kuona mizoga hiyo ikielea majini walipokuwa wakielekea kazini. Viboko hulisha katika maeneo ya kandokando ya ziwa,” alisema. Baadaye, wavuvi wengine waliripoti mizoga miwili katika eneo la Malewa, ambayo ilikuwa imevimba.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.