📰 Newspapers

Mamia kunufaika na mradi wa kiwanda cha Bamburi

Mamia kunufaika na mradi wa kiwanda cha Bamburi

KIWANDA kipya cha kuzalisha kemikali ya kuunda saruji kinachojengwa Matuga, Kaunti ya Kwale, kinatarajiwa kuongeza uwezo wa Bamburi Cement kuzalisha kemikali ya Clinker kutoka tani milioni moja hadi milioni 2.6 kwa mwaka.

Mradi huo wa Sh250 milioni pia utaongeza uwezo wa kampuni hiyo kuzalisha saruji kutoka tani milioni 1.8 hadi milioni nne kila mwaka, hatua inayolenga kuimarisha sekta ya ujenzi nchini na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa hiyo.

Rais William Ruto aliweka jiwe la msingi la mradi huo, uliohudhuriwa na viongozi wa serikali, wawekezaji na viongozi wa eneo hilo.

Miongoni mwa waliohudhuria ni Mawaziri Hassan Joho na Salim Mvurya, Mkurugenzi Mkuu wa Amsons Group Edha Nahdi, Gavana wa Kwale Fatuma Achani, Spika wa Seneti Amason Kingi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bamburi Cement Dkt John Simba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Nahdi alisema uwekezaji huo unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya Amsons Group katika kukuza uchumi wa Kenya na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa nchini.

Kwa upande wake, Dkt Simba alisisitiza umuhimu wa kuhakikisha jamii zinazoishi karibu na mradi zinanufaika na uwekezaji huo.

Alitaja mpango wa kuhamisha wakazi wa Kijiji cha Mwachome, ambao ulihusisha pia mafunzo ya usimamizi wa fedha ili kuwasaidia wakazi walioathiriwa kutumia vizuri rasilimali walizopokea.

Gavana Achani alitoa wito kwa wakazi wa Matuga na wafanyabiashara wa eneo hilo kushirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huo ili wanufaike na…

In brief

KIWANDA kipya cha kuzalisha kemikali ya kuunda saruji kinachojengwa Matuga, Kaunti ya Kwale, kinatarajiwa kuongeza uwezo wa Bamburi Cement kuzalisha kemikali ya Clinker kutoka tani milioni moja hadi milioni 2.6 kwa mwaka. Mradi huo wa Sh250 milioni pia utaongeza uwezo wa kampuni hiyo kuzalisha saruji kutoka tani milioni 1.8 hadi milioni nne kila mwaka, hatua inayolenga kuimarisha sekta ya ujenzi nchini na kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa hiyo.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.