📰 Newspapers

IEBC yakana kufungulia Gachagua mlango kugombea urais 2027

IEBC yakana kufungulia Gachagua mlango kugombea urais 2027

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekanusha madai kwamba imemfungulia njia aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.

Katika taarifa, tume hiyo ilisema bado haijatoa uamuzi wowote kuhusu iwapo Bw Gachagua anastahili kugombea urais au la, ikisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa wakati mwafaka wa mchakato wa uchaguzi.

"Tume haijamuidhinisha wala kutoa uamuzi kuhusu ufaafu wa Mheshimiwa Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi wa 2027. Uamuzi kuhusu ufaafu wa mgombeaji yeyote utafanywa katika hatua inayofaa ya mchakato wa uchaguzi kwa kuzingatia Katiba na sheria husika," ilisema IEBC.

Ufafanuzi huo ulitolewa baada ya Mkurugenzi wa Sheria wa IEBC, Chrispine Owiye, kueleza Jumanne kwamba tume haina mamlaka ya kumzuia mtu kuwania kiti cha kisiasa kwa misingi ya masuala ya uadilifu ikiwa bado ana kesi mahakamani.

Bw Owiye alikuwa akifafanua masharti ya Katiba kuhusu watu wanaostahili au wasiostahili kugombea uchaguzi.

Alisema Mahakama Kuu, kupitia Jaji Anthony Mrima mwaka 2018, iliamua kuwa IEBC haina mamlaka ya kumzuia mtu kuwania uchaguzi kwa misingi hiyo. Hata hivyo, tume ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo na bado inasubiri hukumu.

'Tuna matumaini kwamba tutapata uamuzi utakaotupendelea,' alisema.

Bw Owiye alirejelea Kifungu cha 99(3) cha Katiba kinachosema mtu hawezi kuzuiwa kugombea ubunge hadi uwezekano wote wa kukata rufaa au kuomba mapitio ya hukumu au uamuzi husika uwe umemalizika.

In brief

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekanusha madai kwamba imemfungulia njia aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027. Katika taarifa, tume hiyo ilisema bado haijatoa uamuzi wowote kuhusu iwapo Bw Gachagua anastahili kugombea urais au la, ikisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa wakati mwafaka wa mchakato wa uchaguzi. "Tume haijamuidhinisha wala kutoa uamuzi kuhusu ufaafu wa Mheshimiwa Rigathi Gachagua kuwania urais katika uchaguzi wa 2027.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.