📰 Newspapers

Viongozi wa makanisa wakataa kusitisha kutangaza ibada kwenye runinga na mitandao

Viongozi wa makanisa wakataa kusitisha kutangaza ibada kwenye runinga na mitandao

ONYO la Kamishna wa Ulinzi wa Data anayeondoka, Immaculate Kassait, kwa makanisa kwamba lazima yapate idhini ya waumini kabla ya kutangaza picha zao mubashara, limezua hasira miongoni mwa viongozi wa kidini.

Agizo hilo linataka makanisa kupata ridhaa ya wazi kutoka kwa waumini kabla ya kutangaza ibada mubashara au kuchapisha video na picha zao kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, viongozi wa makanisa wamelipinga wakisema linalenga taasisi za kidini pekee huku shughuli nyingine zinazohusisha upigaji picha na video zikiachwa.

Mwenyekiti wa kitaifa wa Church and Clergy Association of Kenya, Askofu Hudson Ndeda, amehoji kwa nini tume hiyo imeelekeza nguvu zake kwa makanisa pekee ilhali wanasiasa pia hutangaza mikutano yao mubashara.

"Tutatii agizo hilo pale watakapofanya vivyo hivyo kwa mikutano ya kisiasa na maeneo mengine yote ambako video na picha hunaswa, ikiwemo sherehe na vyombo vya habari," alisema Askofu Ndeda.

Ingawa agizo hilo linalenga kuhakikisha taasisi zinafuata Sheria ya Ulinzi wa Data ya mwaka 2019, makanisa yamehoji muda ambao limetolewa. V

iongozi hao wanataka kujua kwa nini kamishna ameamua kutekeleza masharti hayo mwishoni mwa muhula wake.

Askofu Ndeda ameyashauri makanisa kupuuza agizo hilo licha ya hatari ya kutozwa faini ya Sh5 milioni kwa kukosa kupata ridhaa ya waumini.

"Kwa sasa, turuhusiwe kukaidi sheria hiyo ya kibaguzi inayolenga kuingilia tunavyoendesha ibada. Je, kanisa ndilo eneo pekee ambako matangazo mubashara na upigaji picha hufanyika?"…

In brief

ONYO la Kamishna wa Ulinzi wa Data anayeondoka, Immaculate Kassait, kwa makanisa kwamba lazima yapate idhini ya waumini kabla ya kutangaza picha zao mubashara, limezua hasira miongoni mwa viongozi wa kidini. Agizo hilo linataka makanisa kupata ridhaa ya wazi kutoka kwa waumini kabla ya kutangaza ibada mubashara au kuchapisha video na picha zao kwenye mitandao ya kijamii.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.