📰 Newspapers

Sababu za Wakatoliki kuwaombea wafu mwezi Novemba

Sababu za Wakatoliki kuwaombea wafu mwezi Novemba

Kwa Wakatoliki, mwezi Novemba ni kipindi maalumu cha kuwakumbuka na kuwaombea waumini waliofariki, wakiamini kuwa kifo hakikatishi uhusiano wa kiroho kati ya walio hai na waliotangulia mbele ya haki.

Katika kipindi hiki, waumini huombea jamaa, marafiki na watu wengine waliofariki, wakiomba Mungu awasamehe dhambi zao na kuwapa pumziko la milele. Wengine huagiza Misa maalumu, kutembelea makaburi na kutoa sadaka kwa nia ya kuwaombea wapendwa wao.

Ibada hii huanza Novemba 1, Siku ya Watakatifu Wote, ambapo Kanisa huwaheshimu wale wanaoaminiwa kuwa tayari wako mbinguni. Novemba 2 ni Siku ya Waumini Wote Waliokufa, ambapo sala hutolewa kwa marehemu, hasa wale wanaoaminika kuwa katika toharani wakisubiri utakaso kabla ya kuingia mbinguni.

Siku hizi mbili zinaakisi kile Kanisa Katoliki linachokiita Umoja wa Watakatifu. Hii ni imani kwamba kuna uhusiano wa kiroho kati ya waumini walio hai duniani, roho zinazopitia utakaso na wale ambao tayari wako mbinguni.

Ingawa Novemba 2 ndiyo siku rasmi ya kuwakumbuka marehemu, jumuiya nyingi za Wakatoliki huendeleza ibada hiyo katika mwezi mzima kupitia Misa, sala na ziara kwenye makaburi.

Desturi hii inahusishwa na Mtakatifu Odilo, kiongozi wa watawa wa Benedicto, ambaye takriban mwaka 998 alihimiza makao ya watawa aliyokuwa akisimamia kufanya sala, kufunga na Misa kwa ajili ya wafu. Baadaye desturi hiyo ilisambaa katika Kanisa la Magharibi.

In brief

Kwa Wakatoliki, mwezi Novemba ni kipindi maalumu cha kuwakumbuka na kuwaombea waumini waliofariki, wakiamini kuwa kifo hakikatishi uhusiano wa kiroho kati ya walio hai na waliotangulia mbele ya haki. Ibada hii huanza Novemba 1, Siku ya Watakatifu Wote, ambapo Kanisa huwaheshimu wale wanaoaminiwa kuwa tayari wako mbinguni. Ingawa Novemba 2 ndiyo siku rasmi ya kuwakumbuka marehemu, jumuiya nyingi za Wakatoliki huendeleza ibada hiyo katika mwezi mzima kupitia Misa, sala na ziara kwenye makaburi.

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.