📰 Newspapers

MASHAIRI: Charlene Arusi Ilifana

MASHAIRI: Charlene Arusi Ilifana

La leo hili natunga, Charlene kumpongezaKwa yake ndoa kufunga, pasipo cha kutatizaKama mola livopanga, ahadi wakatimizaMwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana Mwanako Ruto arusi, ilifana kwelikweliBintiyo yani rais, kafunga yake halaliMungu bila wasiwasi, liwabariki JalaliMwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana Babake pia mamake, mlikuwa kando yakeKumzawadi manake, yeye na kipenzi chake Naye kweli mama yake, ni…

La leo hili natunga, Charlene kumpongeza

Kwa yake ndoa kufunga, pasipo cha kutatiza

Kama mola livopanga, ahadi wakatimiza

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

Mwanako Ruto arusi, ilifana kwelikweli

Bintiyo yani rais, kafunga yake halali

Mungu bila wasiwasi, liwabariki Jalali

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

Babake pia mamake, mlikuwa kando yake

Kumzawadi manake, yeye na kipenzi chake

Naye kweli mama yake, ni mfano bora kwake

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

Wachache lohudhuria, sana walifurahia

Mavazi ya kuvutia, wote waliyavalia

Viusasa lionea, yote liyoendelea

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

La maua lako koti, nalo chonjo kakuweka

Nzuri nzuri yako suti, mfalme kaoneka

Rachel naye kwa hakika, malkia lipendeka

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

Ingawaje sikuweza, kufika niliwaona

Karamu ilipendeza, mkafurahia sana

Hata densi mlicheza, na Sudi nilimuona

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

Mwanzo wao kule Mwanza, ninaomba mshairi

Maisha wanapoanza, ya ndoa wawe tayari

Beti hizi nawatunza, kuwatakia la heri

Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana

JADIEL MWENDA

"MACHO KUBWA MUONA MBALI"

MAUA, MERU

Sijaumbiwa mbwembwe

Ningaling'aa gizani, palipo mwanga hafifu,

Wengineo watamani, kufikia yangu kifu,

Jambo moja asilani, nalipinga maradufu,

Majigambo na shauo, sijaumbiwa Mirumbe.

Ningaandika vitabu, nivijaze kwenye safu,

Mashairi niratibu, na riwaya timilifu,

Sikubali majaribu, kwangu mja nijisifu,

Majigambo na shauo, sijaumbiwa Mirumbe.

Ningazichangia mada, kwa magazeti tukufu,

In brief

La leo hili natunga, Charlene kumpongeza Kwa yake ndoa kufunga, pasipo cha kutatiza Kama mola livopanga, ahadi wakatimiza Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana Mwanako Ruto arusi, ilifana kwelikweli Bintiyo yani rais, kafunga yake halali Mungu bila wasiwasi, liwabariki Jalali Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana Babake pia mamake, mlikuwa kando yake Kumzawadi manake, yeye na kipenzi chake Naye kweli mama yake, ni mfano bora kwake Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana Wachache lohudhuria, sana walifurahia Mavazi ya kuvutia, wote waliyavalia Viusasa lionea, yote liyoendelea Mwanako Ruto arusi, kule Mwanza ilifana La maua lako koti, nalo chonjo kakuweka Nzuri nzuri yako suti, mfalme k…

This is the opening of the story, shared with credit to Taifa Leo. The rest of the report — with every detail — continues on the publisher’s website.

Continue reading at Taifa Leo ↗

Cookie settings

Choose which cookies we may use. You can change this at any time from Cookie settings in the footer. Details of each cookie are in the Cookie Policy.

Strictly necessary

Needed for sign-in, security, payments and remembering these choices. Always on.

Preferences

Remember settings such as dark mode.

Analytics & performance

Help us count visits, understand which pages, devices and countries our readers use, and measure how well the site performs – anonymous and aggregated.

Advertising & marketing

Lets advertising partners show and personalise adverts, measure impressions, clicks and visits, prevent ad fraud and pay us – this is how the free site is funded.

🔔 News notifications

Get headlines from NewsHub on this device — even when the site is closed.

You can switch this off at any time. Works on Android, Windows, Mac and Linux browsers; on iPhone/iPad add the site to your Home Screen first.